Yakobo 5:7-19
Neno: Bibilia Takatifu
Subira Na Mateso
7 Kwa hiyo, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapo kuja. Angalieni jinsi mkulima anavyongojea ardhi itoe mavuno mazuri, jinsi anavyongojea kwa subira mvua za mwanzo na za mwisho. 8 Hali kadhalika nanyi muwe na subira. Muwe na mioyo tha biti kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia. 9 Ndugu zangu, msi nung’unikiane wenyewe kwa wenyewe, ama sivyo mtahukumiwa. Hakimu amesimama mlangoni.
10 Ndugu zangu, kama mfano wa subira wakati wa mateso, waan galieni manabii walionena katika jina la Bwana. 11 Kama mnavy ojua tunawahesabu kuwa wamebarikiwa wale ambao wamevumilia. Mmek wisha kusikia habari za ustahimilivu wa Ayubu na mmeona shabaha ya Bwana, jinsi Bwana alivyo na huruma na rehema.
12 Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, ama kwa mbingu, au kwa dunia au kwa kiapo kingine cho chote. Bali mkisema ‘Ndio’ iwe ndio, na mkisema ‘Hapana
Maombi Ya Imani
13 Je, kuna mtu ye yote miongoni mwenu aliye na shida? Basi na aombe. Je, yuko mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za sifa. 14 Je, kuna mtu miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta katika jina la Bwana. 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa huyo na Bwana atamwinua. Kama ametenda dhambi, atasamehewa. 16 Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mtu mwenye haki yana nguvu na huleta matokeo.
17 Eliya alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo kwamba mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na nusu. 18 Kisha akaomba tena na mbingu zikatoa mvua na ardhi ikazaa matunda yake.
19 Ndugu zangu, ikiwa mtu miongoni mwenu anapotoka kutoka katika kweli na mtu mwingine akamrejesha,
Read full chapter
Marko 15:33-39
Neno: Bibilia Takatifu
Kifo Cha Yesu Msalabani
33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita
Eliya!”
36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”
37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica