Font Size
Yakobo 5:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yakobo 5:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
5 Mmeishi maisha ya anasa duniani na kujifurahisha na kila kitu mlichotaka. Mmeinenepesha miili yenu, kama wanyama walio tayari kwa siku ya kuchinjwa. 6 Mmehukumu na kuua wale watu wasio na hatia, na ambao hawakupingana nanyi.
Uwe Mstahimilivu
7 Hivyo kina kaka na kina dada, muwe na subira; hadi kuja kwa mara ya pili kwa Bwana. Kumbukeni kuwa mkulima huyasubiria mazao yake yenye thamani yakue ardhini. Huyangoja kwa subira mpaka yapate mvua za masika na za vuli.[a]
Read full chapterFootnotes
- 5:7 mvua za masika na za vuli “Mvua za masika” zilinyesha mwanzoni na “mvua za vuli” zilinyesha mwishoni.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Copyright © 2017 by Bible League International