Font Size
Yakobo 4:11-13
Neno: Bibilia Takatifu
Yakobo 4:11-13
Neno: Bibilia Takatifu
Kuhusu Kuhukumiana
11 Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Mtu anayesema maovu kumhusu ndugu yake au kumhukumu ndugu yake anailaumu sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi hutii sheria bali umekuwa hakimu wa sheria. 12 Ni Mungu peke yake ambaye ametoa sheria na pia yeye ndiye hakimu; ni yeye tu awezaye kuokoa na kuangamiza.
Usijivunie ya Kesho
13 Sasa nisikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae mwaka mmoja huko, tufanye biashara na kuchuma fedha.”
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica