Ulimi pia ni kama moto. Ulimi ni ulimwengu wa uovu kati ya viungo vyetu. Humchafua mtu nafsi nzima na kuwasha moto maisha yake yote, nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu. Wanyama wa kila aina, ndege, nyoka na viumbe vya baharini wanafugwa na wamekwisha kufugwa na binadamu. Lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu unaohangaika huku na kule, uliojaa sumu inayoua.

Read full chapter