Imani Na Matendo

14 Kuna faida gani, ndugu zangu, ikiwa mtu atasema, “Ninayo imani,” na huku hana matendo? 15 Tuseme ndugu fulani au dada hana nguo wala chakula. 16 Ikiwa mmoja wenu atawaambia, “Nendeni salama, mkaote moto na kushiba,” pasipo kuwapatia mahitaji yao ya mwili, kuna faida gani? 17 Vivyo hivyo imani peke yake kama haina matendo, imekufa.

18 Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nita kuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. 19 Unaamini kuwa kuna Mungu mmoja. Vema. Lakini hata mashetani huamini hivyo, nao hutetemeka!

20 Ewe mpumbavu, unataka ushahidi wa kuthibitisha kwamba imani bila matendo ni bure? 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesa biwa haki kwa matendo, alipomtoa mwanae Isaki madhabahuni? 22 Unaona jinsi ambavyo imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake na imani ikakamilishwa kwa matendo. 23 Kwa njia hiyo yaka timizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akahesabiwa kuwa mtu mwenye haki”; naye akaitwa rafiki wa Mungu.

24 Mnaona kwamba mtu huhesabiwa haki kwa matendo wala si kwa imani peke yake. 25 Hali kadhalika Rahabu, yule kahaba, yeye je, hakuhesabiwa haki kwa matendo yake alipowapokea wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? 26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika imani pasipo matendo imekufa.

Read full chapter

Petro Amkana Yesu

66 Petro alikuwa bado yuko barazani. Kisha akaja mtumishi mmoja wa kike wa kuhani mkuu. 67 Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 Lakini Petro akakataa, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema,” akaondoka akaenda mlangoni. 69 Yule mtumi shi wa kike akamwona, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama pale, “Huyu mtu ni mmoja wao.” 70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 71 Petro akaanza kulaani na kuapa, akawaambia, “Simjui huyo mtu mnayemsema.”

72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji Yesu

Read full chapter