20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?

22 Tunajuaje kama Mungu, kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na nguvu yake, amewavumilia kwa uvumilivu mkuu wale waliomkasi risha, ambao wameandaliwa kuangamizwa?

Read full chapter