Tusemeje basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, sivyo! Kama isingekuwapo sheria, nisingalifahamu dhambi ni nini. Hakika nisi ngalijua tamaa ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” Lakini dhambi ilipata nafasi katika amri hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi ime kufa. Kabla ya kuwapo sheria, nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipowasili dhambi nayo ilikuwa hai, nami nikafa.

Read full chapter