Font Size
Warumi 7:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Warumi 7:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
5 Hapo zamani tulitawaliwa na udhaifu wetu wa kibinadamu. Sheria ilitufanya tutake kutenda dhambi. Na tamaa hizo za dhambi ziliitawala miili yetu, na yale tuliyofanya yalituletea mauti ya rohoni. 6 Sasa, kama watu waliokufa, tuko huru kutoka katika sheria iliyotushikilia kama wafungwa. Hivyo hatumtumikii Mungu tena kwa jinsi ya zamani, kwa sheria zilizoandikwa. Sasa tunamtumikia Mungu kwa namna mpya, kwa Roho.
Dhambi na Sheria
7 Mnaweza kudhani ninasema ya kwamba dhambi na sheria vinafanana. Sisemi hivyo. Lakini sheria ilikuwa njia pekee ya kunifundisha maana ya dhambi. Nisingeweza kujua kwamba ni kosa kutamani kitu kisichokuwa changu. Lakini sheria inasema, “Usitamani mali ya mtu mwingine.”(A)
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International