Tulipokuwa tukitawaliwa na hali yetu ya dhambi, tamaa zetu za dhambi zikiwa zinachochewa na sheria, zilikuwa zikifanya kazi katika miili yetu, tukatumikishwa katika huduma ya dhambi ambayo matunda yake ni kifo. Lakini sasa tumekuwa huru kutoka katika kifungo cha sheria kwa kuwa tumekufa kuhusu yale mambo yaliyotu funga, ili tuhudumu katika maisha mapya ya Roho na wala si katika ile njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.

Tusemeje basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, sivyo! Kama isingekuwapo sheria, nisingalifahamu dhambi ni nini. Hakika nisi ngalijua tamaa ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.”

Read full chapter