Warumi 15-16
Neno: Bibilia Takatifu
15 Sisi tulio imara katika imani, hatuna budi kuchukuliana na udhaifu wa wale ambao si imara. Tusitafute kujipendeza wenyewe. 2 Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake ili kumjenga katika imani. 3 Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe bali alikuwa kama ilivyoandikwa: “Matusi yote waliyoku tukana wewe yalinipata mimi.” 4 Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini. 5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 6 ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kuhusu Umoja
7 Mpokeane ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowapokea, ili Mungu apate kutukuzwa. 8 Maana nawaambia kwamba, Kristo alikuwa mtumishi kwa Waisraeli ili kuonyesha kuwa Mungu ni mwaminifu,na kuthibitisha ahadi alizowapa baba zetu. 9 Na pia ili watu wa mataifa mengine wamtukuze Mungu kwa huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko: “Kwa sababu hii nitakutukuza kati ya watu wa mataifa, nitaimba nyimbo za kulisifu jina lako.” 10 Na tena yanasema, “Ninyi watu wa mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.” 11 Na tena: “Msifuni Bwana enyi watu wote wa mataifa, watu wote wamsifu.” 12 Na tena Isaya anasema:“Shina la Yese lita chipuka, atatoka huko atakayetawala mataifa yote; na watu wa ma taifa watamtumaini.”
13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele.
Huduma Ya Paulo Kwa Mataifa
14 Mimi nimeridhika ndugu zangu kuwa ninyi mmejaa wema, mnao ufahamu wote, tena mnaweza kujengana. 15 Lakini kuhusu mambo fulani nimewaandikia kwa ujasiri nikiwa na shabaha ya kuwa kumbusha kwa sababu Mungu amenipa neema maalumu. 16 Amenichagua kuwa mtumishi wa Kristo Yesu kwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu, nitoe huduma ya kikuhani kwa kuitangaza Injili ya Mungu, ili watu wa mataifa wawe sadaka inayokubaliwa na Mungu na iliy otakaswa na Roho Mtakatifu.
17 Kwa hiyo nina sababu ya kujisifu ndani ya Kristo kwa huduma yangu kwa Mungu. 18 Hata sitasema juu ya jambo lo lote isipokuwa katika yale tu ambayo Kristo mwenyewe ameyafanikisha kwa kunitumia, katika maneno na matendo yangu, akawavuta watu wa mataifa wamtii akitumia 19 nguvu za ishara na miujiza, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kuanzia Yerusalemu mpaka kando kando ya Iliriko nimekwisha kuhubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu. 20 Shabaha yangu imekuwa nisihubiri mahali ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwin gine. 21 Lakini kama ilivyoandikwa, “Wale ambao hawajaambiwa habari zake, wataona na wale ambao hawajasikia wataelewa.”
Paulo Apanga Kwenda Roma
22 Hii ndio sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu.
23 Lakini maadamu sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimetamani sana kuja kwenu, 24 natu maini kuwaona nikiwa safarini kwenda Spania, nifurahi kwa muda pamoja nanyi, kisha mnipatie msaada kwa safari hiyo. 25 Ila sasa nakwenda kupeleka msaada kwa watu wa Mungu walioko Yerusalemu. 26 Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yameamua kutoa mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu wasiojiweza walioko huko Yerusalemu. 27 Wamependa kufanya hivyo lakini kwa kweli ni wajibu wao, maana kama watu wa mataifa mengine wameshiriki katika baraka za kiroho za Waisraeli, wanawajibika kuwahudumia Waisraeli katika mahitaji yao ya kimwili. 28 Kwa hiyo baada ya kukamilisha kazi hii na kuhakikisha kuwa wamepokea kila kitu kilichokusanywa, nitakwenda Spania kupitia kwenu. 29 Ninafahamu kwamba nitakapokuja kwenu, nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.
30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, muwe pamoja nami mkiniombea kwa Mungu. 31 Ombeni niepushwe na wale wasioamini walioko Uyahudi, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa na watu wa Mungu; 32 ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, niburudishwe pamoja nanyi. 33 Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.
Salamu Kwa Watu Mbalimbali
16 Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika Kanisa la Kenkrea. 2 Mpokeeni kama dada yenu katika Kristo, jinsi iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wow ote atakaohitaji kutoka kwenu maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, pamoja na mimi.
3 Salamu zangu kwa Priska na Akila, watumishi wenzangu katika huduma ya Kristo Yesu. 4 Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Mimi ninawashukuru wao; na si mimi tu bali pia makanisa yote ya watu wa mataifa mengine. 5 Natoa salamu pia kwa lile kanisa linaloabudu nyumbani kwao. Msalimuni rafiki yangu Epaineto aliyekuwa mtu wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
6 Salamu zangu kwa Maria aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu. 7 Wasalimuni Andronika na Yunia, jamaa zangu ambao wamekuwa gerezani pamoja nami. Wao ni maarufu miongoni mwa mitume, na walimfahamu Kristo kabla yangu. 8 Salamu zangu kwa Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana. 9 Salamu zangu kwa Urbano mfanyakazi mwenzetu katika utumishi wa Kristo pamoja na rafiki yangu mpendwa Stakisi. 10 Salamu zangu kwa Apele ambaye amethibitisha imani yake kwa Kristo. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani kwa Aristobulo. 11 Salamu zangu kwa ndugu yangu Herodioni, na kwa wote walio nyumbani kwa Narkisi wanaomwamini Bwana. 12 Salamu zangu kwa Trifainia na Trifosa, wakina mama wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana. Msalimuni mpendwa wangu Persisi ambaye pia ni mama mwingine aliyemtumikia Bwana kwa bidii. 13 Salamu zangu kwa Rufo, mteule wa Bwana na mama yake, ambaye amekuwa kama mama yangu pia. 14 Wasalimuni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao. 15 Salamu zangu kwa Filologona na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa na watu wote wa Mungu walio pamoja nao. 16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. Ndugu wa makanisa yote ya
Maonyo Ya Mwisho
17 Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na wote wanaoleta mafara kano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea. Waepukeni. 18 Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya, hupo tosha mioyo ya watu wanyofu. 19 Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na nimekuwa na furaha kwa ajili yenu. Lakini napenda muwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu. 20 Na Mungu wa amani hatakawia kumponda shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi. 21 Timotheo, mfanyakazi mwenzangu anawasalimu. Mnasalimiwa pia na Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu. 22 Na mimi Tertio niliyem wandishi wa barua hii nawasalimia kama ndugu yenu katika Kristo. 23 Salamu kutoka kwa Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote la hapa. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto pia wanawasalimu. [ 24 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amina].
Sala Ya Kumsifu Mungu
25 Na asifiwe Mungu ambaye anaweza kuwaimarisha katika Injili niliyowahubiria juu ya Yesu Kristo, kulingana na mafunuo ambayo yalikuwa yamefichika tangu zamani za kale; 26 lakini ambayo sasa yamewekwa wazi na kwa njia ya Maandiko ya manabii yamedhihirishwa kwa mataifa yote kwa amri ya Mungu wa milele, wapate kumwamini na kumtii. 27 Mungu aliye pekee mwenye hekima, atukuzwe milele na milele kwa njia ya Yesu Kristo! Amina.

Copyright © 1989 by Biblica