Kwa maana amri zisemazo: Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 10 Upendo haumfanyii jirani jambo baya, kwa hiyo upendo unakamilisha sheria zote.

11 Fanyeni hivi mkitambua kuwa sasa tumo katika wakati gani. Huu ni wakati wa kuamka kutoka usingizini, kwa maana wokovu wetu umekaribia zaidi sasa kuliko wakati tulipoamini kwa mara ya kwanza.

Read full chapter