Huruma Ya Mungu Kwa Waisraeli

11 Kwa hiyo nauliza, je, Mungu amewakataa watu wake? La, sivyo. Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, wa uzao wa Ibrahimu na wa kabila la Benjamini. Mungu hajawakataa watu wake ambao aliwajua tokea mwanzo. Hamfahamu Maandiko yanavyosema kuhusu Eliya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Waisraeli akisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuziharibu madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua? Na Mungu alimjibuje? “Nime bakiza kwa ajili yangu watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.” Ndivyo ilivyo hata sasa; wapo wachache wal iosalia ambao Mungu amewachagua kwa neema yake. Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, haiwezekani tena wakachaguliwa kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa hivyo, neema isingekuwa neema tena.

Tusemeje basi? Waisraeli walishindwa kupata kile ambacho walikitafutakwa bidii. Lakini waliochaguliwa walikipata. Wa liobaki walifanywa wagumu, kama Maandiko yasemavyo, “Mungu ali wapa mioyo mizito, na macho ambayo hayawezi kuona, na masikio ambayo hayawezi kusikia, hata mpaka leo.” Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa, na kitu cha kuwakwaza waanguke na kuadhibiwa, 10 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, na migongo yao ipinde kwa taabu daima.”

Kurejeshwa Kwa Waisraeli

11 Nauliza tena, je, Waisraeli walipojikwaa walianguka na kuangamia kabisa? La sivyo! Lakini kwa sababu ya uhalifu wao, wokovu umewafikia watu wa mataifa mengine, ili Waisraeli waone wivu. 12 Ikiwa uhalifu wao umeleta utajiri mkubwa kwa ulimwe ngu, na kama kuanguka kwao kumeleta utajiri kwa watu wasiomjua Mungu, basi Waisraeli wote watakapoongoka itakuwa ni baraka kub wa zaidi.

13 Sasa ninasema nanyi watu wa mataifa mengine. Mimi ni mtume kwa watu wa mataifa na ninajivunia huduma hiyo 14 ili kuwafanya Wayahudi wenzangu waone wivu, na hivyo niwaokoe baadhi yao. 15 Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao kumefanya ulimwengu wote upatanishwe na Mungu, kuokolewa kwao je, si kutakuwa ni uhai kutoka kwa wafu? 16 Na kama sehemu ya kwanza ya unga ulioumuliwa ni wakfu, basi unga wote ni wakfu; na kama shina ni wakfu, matawi nayo yatakuwa wakfu.

17 Lakini kama baadhi ya matawi yamekatwa, na ninyi kama mizeituni mwitu mkapandwa katika shina, mkashiriki pamoja na matawi mengine chakula kutoka katika shina la mzeituni, 18 msi jivune mbele ya hayo matawi. Kama mkijisifu mkumbuke kuwa si ninyi mnaoshikilia shina, bali ni shina linalowashikilia ninyi. 19 Pengine mtasema, “Matawi yalikatwa ili nipate nafasi ya kupandikizwa katika shina.” 20 Hii ni kweli. Lakini kumbuka kuwa matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini; na wewe umesimama imara kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijisifu, bali ujinyenyekeze na kuogopa. 21 Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, hatakuacha wewe, atakuondoa. 22 Tafakari basi kuhusu wema na ukali wa Mungu. Yeye ni mkali kwa wale walio anguka, bali amekuonyesha wewe wema wake, kama utadumu katika wema wake. Vinginevyo, na wewe utakatiliwa mbali. 23 Na hata hao Waisraeli, kama wakiacha kudumu katika kutokuamini kwao, atawar udisha kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwarejesha. 24 Ikiwa ninyi mmekatwa kutoka katika mizeituni mwitu, na ki nyume cha asilia mkapandikizwa kwenye mzeituni uliopandwa, ita kuwa ni rahisi kiasi gani matawi haya ya asili kurejeshwa kwenye shina lake?

Huruma Ya Mungu Ni Kwa Wote

25 Ndugu zangu, napenda mfahamu siri hii, msije mkaanza kujiona. Waisraeli wamekuwa na mioyo migumu kwa kiasi fulani mpaka idadi kamili ya watu wa mataifa mengine watakapoamini. 26 Na ndipo Waisrael wote wataokoka kama ilivyoandikwa, “Mko mbozi atakuja kutoka Sayuni, na kuuondoa uasi wote kutoka katika uzao wa Yakobo. 27 Na hii itakuwa ni agano langu nao, nitakapoondoa dhambi zao.”

28 Basi Waisraeli ni maadui wa Mungu kwa sababu ya Injili. Hii ni kwa faida yenu. Lakini kuhusu uchaguzi, Waisraeli bado ni wapendwa wa Mungu kwa sababu ya ahadi yake kwa Abrahmu, Isaki na Yakobo. 29 Kwa maana karama za Mungu na wito wake hazifutiki. 30 Kama ninyi zamani mlivyokuwa mmemwasi Mungu na sasa mmepokea rehema kwa sababu ya kutokutii kwao, 31 hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi kwa ajili ya rehema mliyopata kutoka kwa Mungu, ili wao pia wapate rehema. 32 Kwa maana Mungu amewaachia wana damu wote wawe katika uasi, ili aweze kuwahurumia wote.

Wimbo Wa Shukrani

33 Jinsi utajiri wa Mungu ulivyo mkuu! Hekima yake na maarifa yake hayana mwisho. Njia zake na maamuzi yake hayachu nguziki! 34 Kwa maana ni nani amepata kufahamu mawazo ya Mungu au kuwa mshauri wake? 35 Au ni nani amewahi kumpa cho chote ili arudishiwe? 36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa ajili yake na vyote vinadumu kwake. Utukufu ni wake milele. Amina.