15 Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao kumefanya ulimwengu wote upatanishwe na Mungu, kuokolewa kwao je, si kutakuwa ni uhai kutoka kwa wafu? 16 Na kama sehemu ya kwanza ya unga ulioumuliwa ni wakfu, basi unga wote ni wakfu; na kama shina ni wakfu, matawi nayo yatakuwa wakfu.

17 Lakini kama baadhi ya matawi yamekatwa, na ninyi kama mizeituni mwitu mkapandwa katika shina, mkashiriki pamoja na matawi mengine chakula kutoka katika shina la mzeituni,

Read full chapter