Add parallel Print Page Options

26 Hivyo, kwa kuwa watu hawakumheshimu Mungu, Mungu akawaacha wafuate tamaa zao za aibu. Wanawake wao wakabadili namna ya kujamiiana na wakawatamani wanawake wenzao na wakajamiiana wao kwa wao. 27 Wanaume wakafanya vivyo hivyo. Wakaacha kujamiiana na wanawake kwa mfumo wa asili, wakaanza kuwawakia tamaa wanaume wenzao. Wakafanya mambo ya aibu na wanaume na wavulana. Wakajiletea aibu hii juu yao wenyewe, wakapata yale waliyostahili kwa kutelekeza kweli.

28 Watu hawa waliona kuwa haikuwa muhimu kwao kumkubali Mungu katika fikra zao. Hivyo Mungu akawaacha wayafuate mawazo yao mabaya. Hivyo hufanya mambo ambayo mtu yeyote hapaswi kufanya.

Read full chapter