26 Kwa hiyo, Mungu aliwaachia wafuate tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao waliacha matumizi ya asili ya maumbile yao wakatumia miili yao isivyokusudiwa. 27 Hali kadhalika wanaume waliacha uhusiano wa asili kati ya waume na wake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume walifanyiana mambo ya aibu, nao waka pata katika miili yao adhabu waliyostahili kama matokeo ya uovu wao.

28 Zaidi ya hayo, kwa sababu walikataa kumtambua Mungu, yeye aliwaacha katika nia zao za upotovu watende mambo yasiyosta hili kutendwa.

Read full chapter