Add parallel Print Page Options

17 Ndiyo, wema wa uaminifu wa Mungu umedhihirishwa katika Habari Njema kwa uaminifu wa mmoja, ambao huongoza imani ya wengi. Kama Maandiko yanavyosema, “Aliye na haki mbele za Mungu[a] ataishi kwa imani.”[b]

Mungu ni Mwaminifu Na Atauadhibu Uovu

18 Mungu huonesha hasira yake kutokea mbinguni dhidi ya mambo mabaya ambayo waovu hutenda. Hawamheshimu na wanatendeana mabaya. Maisha yao maovu yanasababisha ukweli kuhusu Mungu usijulikane. 19 Hili humkasirisha Mungu kwa sababu wamekwisha oneshwa Mungu alivyo. Ndiyo, Mungu ameliweka wazi kwao.

20 Yapo mambo yanayoonekana kuhusu Mungu, kama vile nguvu zake za milele na yale yote yanayomfanya awe Mungu. Lakini tangu kuumbwa kwa ulimwengu, mambo haya yamekuwa rahisi kwa watu kuyaona. Maana yake ni kuwa, watu wanaweza kumwelewa Mungu kwa kuangalia yale aliyoumba. Hivyo watu hawana udhuru kwa uovu wanaotenda.

21 Watu walimjua Mungu, lakini hawakumheshimu kama Mungu. Na hawakumpa shukrani. Badala yake waliyageukia mambo ya hovyo yasiyo na manufaa. Akili zao zilichochanganyikiwa zilijaa giza. 22 Walisema kuwa wana hekima, lakini wakawa wajinga. 23 Hawakuuheshimu ukuu wa Mungu, anayeishi milele. Wakaacha kumwabudu Mungu wakaanza kuabudu sanamu, vitu vilivyotengenezwa vikaonekana kama wanadamu, ambao wote mwisho hufa, au kwa mfano wa ndege na wanyama wanaotembea na wanaotambaa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:17 Aliye na haki mbele za Mungu Au “Mwenye haki”, mara nyingi hutumika kama cheo cha Masihi, Mfalme Mteule wa Mungu aliyeahidiwa katika Agano la Kale. Tazama Isa 53:11; Hab 2:4; Zek 9:9; Mdo 3:14; 7:52; 22:14.
  2. 1:17 ataishi kwa imani katika Hab 2:4, ambayo pia, inaweza kutafsiriwa kuwa, “Mwenye haki ataishi kwa uaminifu.”