Kutoka kwa Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo na mtume niliyecha guliwa na kuitwa kuhubiri Habari Njema ya Mungu. Habari hii aliiahidi tangu zamani kwa njia ya manabii wake katika Maandiko matakatifu.

Habari hii njema ni kuhusu Mwana wa Mungu ambaye kimwili alizaliwa katika ukoo wa Daudi, na ambaye alidhihiri shwa kuwa Mwana wa Mungu kwa uwezo wa Roho wa utakatifu kwa kufufuliwa kutoka kwa wafu. Yeye ndiye Yesu Kristo Bwana wetu, ambaye kutoka kwake, na kwa ajili yake, tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii. Ninyi pia ni miongoni mwa watu walioitwa kuwa wafuasi wa Yesu Kristo.

Basi, nawatakieni ninyi nyote mlioko huko Roma, ambao ni wapendwa wa Mungu mlioitwa muwe watakatifu, neema na amani ito kayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Maombi Na Shukrani

Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote. Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote ninapo hubiri Habari Njema ya Mwanae, anajua jinsi ninavyowakumbuka siku zote 10 katika sala zangu kila ninapoomba. Namwomba Mungu, akipenda, hatimaye sasa nipate nafasi ya kuja kwenu. 11 Ninata mani sana kuwaona ili niwagawie zawadi ya kiroho ya kuwaima risha, 12 yaani tuimarishane: mimi nitiwe moyo kwa imani yenu na ninyi mtiwe moyo kwa imani yangu.

13 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimeku sudia kuja kwenu, ingawa mpaka sasa nimezuiliwa. Ningependa kupata mavuno ya waamini kati yenu kama nilivyofanikiwa kupata waamini kati ya watu wa mataifa mengine.

14 Ninawajibika kwa watu wote, Wagiriki na wasiokuwa Wagi riki; wenye elimu na wasiokuwa na elimu. 15 Ndio maana ninata mani sana kuhubiri Injili kwenu ninyi pia mlioko Roma.

16 Mimi siionei aibu Injili kwa maanani nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia. 17 Kwa maana Habari hii Njema inaonyesha wazi haki inayotoka kwa Mungu. Haki hii hupatikana kwa imani tangu mwanzo hadi mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Wenye haki wataishi kwa imani.”

Ghadhabu Ya Mungu Kwa Wanadamu

18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wa wanadamu ambao kwa uovu wao wanauficha ukweli usijulikane. 19 Kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao kwa sababu Mungu mwenyewe ameyaweka wazi. 20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.

21 Ingawa walimjua Mungu, hawakumpa heshima na utukufu anaostahili wala kumshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao zilizopumbaa zikatiwa giza. 22 Wakijidai kuwa ni werevu, wakawa wajinga. 23 Wakauacha utukufu wa Mungu aishiye milele wakageukia sanamu zinazofanana na mwanadamu ambaye hufa, na ndege na wanyama na viumbe vitambaavyo.

24 Kwa hiyo, Mungu aliwaacha waendelee kufuata tamaa mbaya za mioyo yao na kutenda matendo ya unajisi nakufanyiana mambo ya aibu katika miili yao. 25 Hii ni kwa sababu walikataa ukweli ku husu Mungu wakaamua kuamini uongo; wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba ahimidiwaye milele! Amina.

26 Kwa hiyo, Mungu aliwaachia wafuate tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao waliacha matumizi ya asili ya maumbile yao wakatumia miili yao isivyokusudiwa. 27 Hali kadhalika wanaume waliacha uhusiano wa asili kati ya waume na wake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume walifanyiana mambo ya aibu, nao waka pata katika miili yao adhabu waliyostahili kama matokeo ya uovu wao.

28 Zaidi ya hayo, kwa sababu walikataa kumtambua Mungu, yeye aliwaacha katika nia zao za upotovu watende mambo yasiyosta hili kutendwa. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na husuda, uuaji, fitina, hadaa, nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 30 wasingiziaji, wanaomchukia Mu ngu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno; wenye hila, wasiotii wazazi wao; 31 niwajinga, wasioamini, wasio na huruma nawaka tili. 32 Ingawa wanafahamu sheria ya Mungu kwamba watu wanaoishi maisha ya namna hii wanastahili mauti, bado wanaendelea kutenda mambo haya na kuwasifu wengine wafanyao kama wao.

Hukumu Ya Mungu

Kwa hiyo huna udhuru wo wote, hata ukiwa nani, unapowahu kumu wengine. Kwa maana unapowahukumu wengine unajihukumu mwe nyewe, kwa kuwa wewe uliye hakimu unafanya mambo hayo hayo. Tunajua kwamba hukumu ya Mungu huwafikia kwa halali wote wanaotenda mambo haya. Je, wewe uliye binadamu tu, unapowahuku mu watu wanaofanya mambo hayo na huku wewe mwenyewe pia unafanya hayo hayo, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? Au labda unad harau wingi wa huruma, uvumilivu na subira ya Mungu, ukasahau kwamba wema wake una shabaha ya kukufanya utubu?

Lakini kwa sababu ya ugumu na ukaidi wa moyo wako usioku bali kutubu, unajiwekea ghadhabu kwa siku ile ambapo ghadhabu ya Mungu na hukumu yake ya haki itadhihirishwa. Siku hiyo, Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake. Wale ambao hutenda wema wakati wote na kutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyo haribika, Mungu atawapa uzima wa milele. Lakini wote watafu tao kujinufaisha, wanaokataa kweli na kufuatauovu, watapokea ghadhabu na hasira ya Mungu. Kwa maana kila binadamu atendaye uovu atapata mateso na shida, kuanzia kwa Myahudi na kisha kwa mtu wa mataifa mengine. 10 Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wote watendao mema; Wayahudi kwanza na kisha watu wa mataifa mengine. 11 Kwa maana Mungu hana upendeleo.

12 Watu wote waliotenda dhambi pasipokuwa na sheria ya Musa wataangamia pasipo sheria; na wale wote waliotenda dhambi chini ya sheria ya Musa watahukumiwa kwa sheria iyo hiyo. 13 Kwa maana wanaohesabiwa haki mbele ya Mungu si wale wanaosikia bali ni wal ewanaotii maagizo ya sheria. 14 Watu wa mataifa mengine ambao hawana sheria ya Musa, wanapoamua kutenda yale ambayo yameagizwa na sheria kwa kuongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa wamejiwekea sheria, ingawa hawana sheria ya Musa. 15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea. 16 Kwa hiyo, kama Habari Njema ninay ohubiri inavyosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile ambayo Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, atayahukumu mawazo ya siri ya wanadamu.

Wayahudi Na Sheria Ya Musa

17 Na wewe je? Wewe unayejiita Myahudi: unaitegemea sheria ya Musa na kujisifia uhusiano wako na Mungu; 18 unajua mapenzi ya Mungu na unatambua lililo bora kutokana na hiyo sheria. 19 Kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walioko gizani; 20 mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una hakika kwamba ndani ya hiyo sheria mna maarifa na kweli yote: 21 wewe unayewafundisha wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe unayehubiri kwamba watu wasiibe, wewe huibi? 22 Wewe unayewaambia watu wasizini, wewe huzini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, huibi katika mahekalu? 23 Wewe unayejisifia sheria, humwaibishi Mungu kwa kuvunja sheria? 24 Kwa maana Maandiko yanasema, “Kwa ajili yenu ninyi Wayahudi, jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa mataifa ya watu wasiom jua Mungu.”

25 Kutahiriwa kuna thamani tu iwapo unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, umekuwa kama hukutahiriwa. 26 Kwa hiyo kama watu ambao hawakutahiriwa wanatimiza maagizo ya she ria, je, Mungu hatawahesabu kuwa kama waliotahiriwa? 27 Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanatii sheria watawa hukumu ninyi mlio na Maandiko ya sheria nakutahiriwa lakini mna vunja sheria. 28 Kwamaana Myahudi wa kweli si yule anayeonekana kwa dalili za nje, wala tohara ya kweli si kitu cha kimwili. 29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ya kweli ni jambo la moyoni, jambo la kiroho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa jinsi hii anapata sifa kutoka kwa Mungu, wala si kutoka kwa wanadamu.

Uaminifu Wa Mungu

Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Je, kutahiriwa kuna faida yo yote? Ndio, zipo faida nyingi. Kwanza, Mungu aliwaka bidhi Wayahudi maagizo yake. Na hata kama baadhi yao hawaku amini,je, kutokuamini kwao kutamfanya Mungu aache kuwa mwaminifu? Hata kidogo!Mungu ataendelea kuwa wa kweli hata kama kila mwan adamu atakuwa mwongo. Kama ilivyoandikwa katika Maandiko,“Wewe Mungu, uthibitishwe kuwa wahaki katika maneno yako, na mshindi katika hukumu.”

Lakini iwapo uovu wetu unadhihirisha wazi kwamba Mungu ni mwenye haki, tusemeje basi? Je, tuseme kuwa Mungu hana haki kutuadhibu? Hapa ninasema kibinadamu. La hasha! Mun gu ana haki kabisa kutughadhibikia! Kama sivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? Mtu anaweza kusema,“Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?” Kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili wema udhihirike”? Hakika hukumu wanayoipata ni ya haki.

Wote Wametenda Dhambi

Tusemeje basi? Sisi Wayahudi tunayo nafuu yo yote? Hata kidogo! Kama tulivyokwisha kusema, Wayahudi na Wagiriki, wote wanatawaliwa na nguvu ya dhambi. 10 Kama Maandiko yase mavyo:“Hakuna hata mmoja mwenye haki; 11 hakuna hata mmoja mwe nye kuelewa, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu. 1 2Wote wamepotoka na kwa pamoja hawana thamani yo yote; hakuna atendaye mema hata mmoja. 13 Makoo yao ni kama makaburi wazi, wanatumia ndimi zao kudanganya. Kwenye midomo yao mnasumu kama ya nyoka. 14 Vinywa vyao vimejaa laana na ukali. 15 Miguu yao huen da mbio kumwaga damu, 16 njia zote wanazopita huacha uharibifu na huzuni kuu, na 17 wala njia ya amani hawaifahamu. 18 Kumcha Mungu hakupo machonipao.”

Mungu hakupo machonipao.”

19 Basi tunafahamu ya kwamba maagizo yote ya sheria ya Musa yanawahusu wale walio chini ya sheria hiyo. Kusudi la sheria ni kuwafanya watu wote wasiwe na kisingizio na kuuweka ulimwengu wote chini ya hukumu ya Mungu. 20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue dhambi.

Haki Kwa Njia Ya Imani

21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua, 23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo. 25 Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani. 26 Pia alifanya hivi ili kuonyesha kwa wakati huu kuwa yeye ni wa haki na kwamba yeye ndiye anayewahesabia haki watu wote wamwaminio Yesu.

Umuhimu Wa Kuwa Na Imani

27 Sasa kujivuna kwetu kuko wapi basi? Hakupo. Je kumeondo lewa kwa msingi gani? Kwa msingi wa kutimiza sheria? La. Kumeon dolewa kwa msingi wa imani. 28 Kwa maana tunasisitiza kwamba mwanadamu anahesabiwa haki kwa njia ya imani na wala si kwa kutenda maagizo ya sheria. 29 Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa mataifa mengine pia? Ndio, yeye ni Mungu wa watu wa mataifa mengine pia. 30 Basi kwa kuwa Mungu ni mmoja, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kutokana na imani yao na wale wasiotahiriwa kutokana na imani yao. 31 Je, ina maana kwamba tunaifuta sheria kwa imani hii? La, sivyo. Kiny ume chake: tunaithibitisha sheria.

Mfano Wa Abrahamu

Tusemeje basi kuhusu baba yetu Abrahamu? Yeye alijifunza nini? Ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, basi anacho kitu cha kujivunia, lakini si mbele za Mungu. Maandiko yanase maje? “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa ajili ya imani yake aka hesabiwa haki.”

Mtu akifanya kazi, mshahara wake hauhesabiwi kuwa ni zawadi bali ni haki yake. Lakini kwa mtu ambaye hakufanya kazi ila amemtegemea Mungu anayewahesabia haki waovu, imani yake inahesabiwa kuwa haki. Daudi pia ana maana hiyo hiyo anapoongea juu ya baraka apatazo mtu ambaye Mungu amemhesabia haki pasipo kutenda lo lote: “Wamebarikiwa wale ambao makosa yao yamesame hewa, ambao dhambi zao zimefunikwa. Amebarikiwa mtu ambaye Bwana hamhesabii dhambi zake.”

Haki Kabla Ya Tohara

Je, baraka hii anayosema Daudi ni ya wale waliotahiriwa tu au pia ni ya wale wasiotahiriwa? Tunasema kwamba imani ya Abra hamu ilihesabiwa kama haki. 10 Je, hii ilitokea wakati gani? Je, ilikuwa ni kabla au baada ya kutahiriwa kwake? Haikuwa baada, ila kabla hajatahiriwa. 11 Na alipewa tohara kama alama na mhuri wa haki aliyoipokea kwa imani hata kabla ya kutahiriwa. Shabaha ya Mungu ilikuwa kwamba Abrahamu awe baba ya wote wenye imani ambao bado hawajatahiriwa ili wao pia wahesabiwe haki. 12 Pia yeye ni baba wa wale waliokwisha kutahiriwa ambao si kwamba wametahiriwa tu, bali pia wanafuata mfano wa imani aliyokuwanayo baba yetu

Haki Haipatikani Kwa Sheria

13 Ahadi ambayo Mungu alimpa Abrahamu na kizazi chake, kwamba ataurithi ulimwengu, haikutolewa kwa kuwa Abrahamu alitii sheria lakini ni kwa sababu alikuwa na imani, na Mungu akaihesabu imani yake kuwa ni haki. 14 Ikiwa wafuatao sheria tu ndio wata kaopewa urithi ulioahidiwa na Mungu, basi imani si kitu na ahadi hiyo haina thamani. 15 Kwa maana sheria huleta ghadhabu ya Mungu na ambapo hakuna sheria basi hakuna makosa.

16 Ndio maana ahadi hiyo ilitolewa kwa msingi wa imani, ili ipatikane bure kwa neema na ithibitishwe kwa vizazi vyote vya Abrahamu, si wale tu walio na sheria, bali pia na wale wenye imani ya Abrahamu. Kwa maana yeye ni baba yetu sote. 17 Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu aliyemwamini. Mungu ambaye ana wapa wafu uhai na ambaye huamuru vitu ambavyo havipo viwepo.

Mfano Wa Imani Ya Abrahamu

18 Ijapokuwa ilionekana kama matumaini ya Ibrahimu yalikuwa ya bure, yeye alimtumaini na kumwamini Mungu na kwa kufanya hivyo akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyokuwa ameahidiwa kwamba, “Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.” 19 Ijapokuwa mwili wake hau kuwa tena na uwezo wa kuzaa, alikuwa na umri upatao miaka mia moja na Sara alishapita umri wa kuzaa, imani yake haikufifia. 20 Abrahamu hakuacha kuamini wala hakuwa na mashaka juu ya ahadi ya Mungu. Imani yake ilimtia nguvu, akamtukuza Mungu, 21 akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza ali loahidi. 22 Ndio sababu imani yake, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.” 23 Maneno haya, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki,” hay akuandikwa kwa ajili yake peke yake 24 bali kwetu pia. Tutahe sabiwa haki sisi tunaomwamini Mungu aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka kwa wafu. 25 Yesu aliuawa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuliwa ili tuhesabiwe haki.

Kuwa Na Amani Na Mungu

Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa kupitia kwake tumepata njia ya kufikia neema hii ambayo inatuwezesha kusimama imara, tukifurahia tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. Zaidi ya hayo, pia tunafurahia mateso yetu kwa sababu tunafahamu kuwa mateso huleta subira; na subira huleta uthabiti wa moyo; na uthabiti wa moyo hujenga tumaini. Tukiwa na tumaini hatuwezi kukata tamaa kwa sababu Mungu amekwisha kumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi tuliyopewa na Mungu.

Tulipokuwa tungali wanyonge, wakati aliochagua Mungu, Kristo aliwafia wenye dhambi. Ni vigumu sana kwa mtu kujitolea kufa kwa ajili ya mwenye haki, ingawa yawezekana mtu akajitolea kufa kwa ajili ya mtu mwema. Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.

Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, bila shaka atatuokoa kutoka katika ghadhabu ya Mungu. 10 Kwa kuwa kama tulipokuwa maadui wa Mungu tulipatanishwa kwa kifo cha Mwanae, bila shaka sasa kwa kuwa tumepatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake. 11 Si hivyo tu, bali pia tunamfurahia Mungu katika Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa ajili yake tumepokea upatanisho wetu.

Adamu Alileta Kifo, Yesu Ameleta Uzima

12 Kwa hiyo kama vile ambavyo dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na dhambi ikaleta kifo, na kwa njia hiyo kifo kikawajia watu wote kwa kuwa wote walitenda dhambi -

13 kwa maana kabla sheria haijatolewa dhambi ilikuwepo ulimwenguni. Lakini dhambi haihesabiwi ambapo hakuna sheria. 14 Hata hivyo tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Musa, kifo kiliwatawala watuwote hata wale ambao dhambi zao hazikuwa kama uasi wa Adamu. Adamu alikuwa mfano wa yule ambaye angalikuja. 15 Lakini zawadi iliyotolewa bure haiwezi kulinganishwa na ule uasi. Kwa maana ikiwa watu wengi walikufa kwa sababu ya uasi wa mtu mmoja, basi neema ya Mungu na zawadi iliyotolewa kwa ajili ya mtu mmoja, Yesu Kristo, imemiminika kwa wingi zaidi kwa watu wengi. 16 Pia zawadi ya Mungu sio kama matukio ya ile dhambi ya mtu mmoja. Kwa maana hukumu iliyotokana na uasi huo ilileta laana, lakini zawadi iliyopatikana bure baada ya dhambi nyingi, inaleta haki ya Mungu. 17 Na ikiwa kutokana na uasi wa mtu mmoja kifo kilitawala kupitia huyo mtu mmoja, wale wanaopokea wingi wa neema na zawadi ya bure ya kuhesabiwa haki, watatawala zaidi sana katika maisha kwa ajili ya huyo mtu mmoja, Yesu Kristo. 18 Kwa hiyo, kama vile uasi wa mtu mmoja ulivyoleta hukumu kwa watu wote, hali kadhalika, tendo la haki la mtu mmoja linawafanya watu wote waachiliwe huru na kupewa uzima. 19 Na kama vile ambavyo watu wengi walifanywa kuwa wenye dhambi kwa ajili ya kutokutii kwa mtu mmoja, vivyo hivyo wengi watahesabiwa haki na Mungu kwa ajili ya utii wa mtu mmoja.

20 Sheria ililetwa ili dhambi iongezeke. Lakini dhambi ili poongezeka, neema iliongezeka zaidi. 21 Kama vile ambavyo dhambi ilitawala kwa njia ya kifo, vivyo hivyo neema ya Mungu iweze kutawala kwa njia ya haki, ikileta uzima wa milele katika Yesu

Uhai Katika Kristo

Tusemeje basi? Tuendelee kutenda dhambi ili neema izidi kuongezeka? Hata kidogo! Itawezekanaje sisi tuliokufa kwa mambo ya dhambi, tuendelee tena kuishi humo? Au hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? Kwa hiyo tulikufa na kuzikwa naye kwa njia ya ubatizo ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa nguvu na utukufu wa Baba, sisi pia tupate kuishi maisha mapya.

Kwa maana ikiwa tumeunganika naye katika kifo chake, basi tutaunganika naye katika kufufuka kwake. Tunafahamu kwamba mwili wetu wa asili ulisulubiwa msalabani pamoja na Kristo ili mwili wetu wa dhambi uharibiwe kabisa na tusiwe tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi. Lakini ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. Kama tujuavyo, Kristo alikwisha kufufu liwa kutoka kwa wafu kwa hiyo hafi tena; kifo hakina mamlaka juu yake tena. 10 Alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, lakini maisha anayoishi anamwishia Mungu.

11 Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kujihesabu kuwa wafu kwa mambo ya dhambi bali hai kwa Mungu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.

12 Basi, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ambayo ni ya muda, iwafanye mzifuate tamaa za mwili. 13 Msiku bali kutoa sehemu yo yote ya miili yenu itumike kama vyombo vya uovu kutenda dhambi. Bali jitoeni kwa Mungu kama watu waliotolewa kutoka katika kifo wakaingizwa uzimani. Pia toeni sehemu zote za miili yenu zitumike kama vyombo vya haki. 14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu kwa sababu hamtawaliwi na sheria bali mnatawaliwa na neema. Watumwa Wa Haki

15 Tufanyeje basi? Tuendelee kutenda dhambi kwa kuwa hatutawa liwi na sheria bali tuko chini ya neema? La , sivyo! 16 Hamfahamu kuwa kama mkijitoa kumtumikia mtu na kumtii kama watumwa basi mnakuwa watumwa wa huyo mnayemtii? Mnaweza kuwa watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti au mnaweza kuwa watumwa wa utii ambao huleta haki. 17 Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao mlikuwa watumwa wa dhambi mmetii kwa moyo wote mafundi sho mliyopewa. 18 Mmewekwa huru, mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa haki. 19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu wenu wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa ajili ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.

20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 21 Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni kifo. 22 Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru kutokana na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakaso, na hatimaye, uzima wa milele. 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Mkristo Hafungwi Na Sheria

Ndugu zangu, kwa kuwa sasa ninasema na wale wanaoifahamu sheria, bila shaka mnaelewa kwamba mtu akifa hafungwi tena na sheria. Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa hufungwa kisheria kwa mumewe wakati wote mumewe akiwa hai. Lakini mumewe akifa mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa. Endapo mwanamke huyo ataishi namwanaume mwingine wakati mumewe yu hai, ataitwa mzinzi. Lakini mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na she ria ya ndoa, na akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.

Kazi Ya Sheria

Kadhalika ndugu zangu, ninyi pia mmekufa kuhusu maagizo ya sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Sasa ninyi ni mali yake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili tumzalie Mungu matunda. Tulipokuwa tukitawaliwa na hali yetu ya dhambi, tamaa zetu za dhambi zikiwa zinachochewa na sheria, zilikuwa zikifanya kazi katika miili yetu, tukatumikishwa katika huduma ya dhambi ambayo matunda yake ni kifo. Lakini sasa tumekuwa huru kutoka katika kifungo cha sheria kwa kuwa tumekufa kuhusu yale mambo yaliyotu funga, ili tuhudumu katika maisha mapya ya Roho na wala si katika ile njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.

Tusemeje basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, sivyo! Kama isingekuwapo sheria, nisingalifahamu dhambi ni nini. Hakika nisi ngalijua tamaa ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” Lakini dhambi ilipata nafasi katika amri hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi ime kufa. Kabla ya kuwapo sheria, nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipowasili dhambi nayo ilikuwa hai, nami nikafa. 10 Ile amri iliyokusudiwa kuleta uzima, ilileta kifo. 11 Dhambi ilipata nafasi katika amri, ikanidanganya, na kwa kutumia amri, ikaniletea kifo.

12 Kwa hiyo sheria yenyewe ni takatifu na amri ni takatifu, na ya haki, tena ni njema.

13 Je, hii ina maana kwamba sheria ambayo ni njema ilinile tea kifo? La, sivyo. Lakini ili dhambi itambuliwe kuwa ni dhambi, iliniletea kifo kwa njia ya sheria ambayo ni nzuri; kusudi kwa njia ya sheria, dhambi ionekane kuwa mbaya kabisa.

Mgongano Kati Ya Mwili Na Roho

14 Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya. 16 Kwa hiyo kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, hii ina maana kwamba nakubali kuwa sheria ni njema. 17 Basi, kwa kweli si mimi hasa nitendaye lile nisilolipenda bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna wema wo wote ndani yangu mimi, yaani katika mwili wangu wa asili. Ingawa nina nia ya kutenda lililo jema, lakini ninashindwa kulitenda. 19 Sitendi lile jema nipendalo bali lile ovu nisilopenda, ndilo nitendalo. 20 Basi kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Kwa hiyo imekuwa kama ni sheria: kila ninapotaka kufanya jambo jema, jambo ovu hujitokeza. 22 Kwa maana ndani yangu ninaifurahia sheria ya Mungu. 23 Lakini ninaona kuna sheria nyin gine mwilini mwangu inayopingana na ile sheria ninayoikubali akilini mwangu. Sheria hii inanifanya kuwa mateka wa sheria ya dhambi ambayo inafanya kazi mwilini mwangu.

24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa na huu mwili wa kifo? 25 Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa hiyo basi, mimi kwa moyo wangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu wa asili ninaitumikia sheria ya dhambi.

Maisha Ya Kiroho

Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.

Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .

Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.

14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu. 15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.

Utukufu Ujao

18 Nayahesabu mateso tunayopata sasa kuwa si kitu yakilin ganishwa na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19 Viumbe vyote vinangoja kwa hamu kudhihirishwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vilifanywa kuwa duni kabisa, si kwa kupenda kwake, bali kwa mapenzi ya Mungu; hata hivyo kulikuwa na matumaini 21 kwamba siku moja viumbe vyote vitawekwa huru kutoka katika utumwa wa kuharibika na vipewe uhuru na utukufu wa watoto wa Mungu.

22 Tunajua kwamba mpaka sasa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa uchungu mkali kama ule wa uzazi. 23 Na si hivyo tu, hata sisi ambao tuna matunda ya kwanza ya Roho tunalia kwa uchungu tukisu biri kwa hamu kufanywa kuwa wana wa Mungu, miili yetu itakapowek wa huru kabisa.

24 Kwa maana tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alichonacho? 25 Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatunacho, basi tunakingoja kwa subira.

26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na mapenzi ya Mungu. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya hivyo kwa faida yao. 29 Wale ambao Mungu alikwisha kuwachagua tangu mwanzo, pia aliwateua wafanane na Mwanae, ili Mwana awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale ambao Mungu aliwateua tangu awali pia ali waita; na wale aliowaita pia aliwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki aliwapa utukufu wake.

Upendo Wa Mungu

31 Tuseme nini basi kuhusu haya yote? Ikiwa Mungu yuko upande wetu ni nani atakayetupinga? 32 Ikiwa Mungu hakumwacha Mwanae bali alimtoa kwa ajili yetu sote, hatatupatia pamoja na Mwanae, vitu vyote? 33 Ni nani atawashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ambaye anawahesabia kuwa hawana hatia. 34 Ni nani basi atakayewahukumu? Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyekufa, na zaidi ya hayo, yeye ndiye aliyefufuliwa akawa hai, na ambaye sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, naye anatuombea. 35 Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo? Ni shida? Au taabu? Au mateso? Au njaa? Au umaskini? Au hatari? Au Kifo? Hapana. 36 Kama Maandiko yasemavyo: “Kwa aji li yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.” 37 Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda. 38 Kwa maana nina hakika kuwa, si kifo wala uzima; si malaika wala mashetani; si mambo ya sasa wala mambo yajayo au mamlaka nyingineyo yote; 39 si mambo yaliyo juu wala yaliyo chi ni sana; wala hakuna kitu kingine cho chote kati ya vitu vyote alivyoumba Mungu kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.

Nafasi Ya Pekee Ya Waisraeli

Ninasema kweli katika Kristo na dhamiri yangu inanishuhudia kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwa sisemi uongo. Nina huzuni sana na uchungu usiokwisha moyoni mwangu. Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Kristo kama kufanya hivyo kungeweza kuwasaidia ndugu zangu tulio wa kabila moja. Nazungumza kuhusu Waisraeli ambao Mungu aliwateua kuwa wana wake, wakapewa utukufu wake, maagano yake, sheria yake, ibada ya kweli, na ahadi zake. Wao ni wa uzao wa mababu wa kwanza, na katika taifa lao Kristo alitoka kama mwanadamu; yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, atukuzwaye milele! Amina.

Lakini hii haina maana kwamba ahadi ya Mungu kwa wana wa Israeli imeshindwa. Kwa maana si wote ambao ni wa uzao wa Israeli ambao ni wa Israeli. Wala si wazaliwa wote wa kizazi cha Abra hamu ambao ni watoto wake. Ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ilikuwa: “Watoto wako watatoka katika uzao wa Isaki.” Kwa maneno men gine, si wale watoto waliozaliwa na Ibrahimu kimwili ambao ni wana wa Mungu; bali ni wale watoto wa ahadi ambao wanahesabiwa kuwa kizazi cha Abrahamu. Kwa maana ahadi yenyewe ilisema, “Nitarudi tena wakati kama huu na Sara atapata mtoto wa kiume.”

10 Na si hivyo tu bali pia wakati Rebeka alipozaa watoto na mume mmoja, Isaki, 11 hata kabla watoto wake mapacha hawajazal iwa wala kutenda jema au baya ili mpango wa Mungu wa kuchagua uendelee, si kwa kutegemea matendo mema bali kwa kufuatana na wito wake - 12 Rebeka aliambiwa, “Mkubwa atamhudumia mdogo.” 13 Kama Maandiko yasemavyo: “Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.”

Mungu Hana Upendeleo

14 Tusemeje basi? Kwamba Mungu ana upendeleo? La, sivyo. 15 Kwa maana Mungu alimwambia Musa, “Nitamrehemu nipendaye kumrehemu; na nitamhurumia nipendaye kumhurumia.” 16 Kwa hiyo haitegemei mapenzi ya mtu au jitihada ya mtu, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17 Kwa maana katika Maandiko Farao anaambiwa, “Nilikuinua kwa makusudi ya kudhihirisha nguvu zangu kwako na jina langu lipate kutangazwa duniani pote.” 18 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia mtu ye yote apendaye kumhurumia na huufanya mgumu moyo wa mtu ye yote atakaye.

19 Bila shaka mtaniuliza, “Kama ni hivyo, kwa nini Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kushindana na mapenzi yake? 20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?

22 Tunajuaje kama Mungu, kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na nguvu yake, amewavumilia kwa uvumilivu mkuu wale waliomkasi risha, ambao wameandaliwa kuangamizwa? 23 Na tunajuaje kama Mungu alifanya hivi ili kuwadhihirishia utajiri wa utukufu wake wale anaowahurumia, ambao aliwaandaa tangu mwanzo kupokea utu kufu? 24 Na sisi ndio hao walioitwa, si kutoka kwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko

25 Hivi ndivyo Mungu asemavyo katika kitabu cha Hosea, “Wale ambao hawakuwa watu wangu, nitawaita ‘watu wangu,’ na wale ambao hawakuwa wapendwa wangu, nitawaita ‘wapendwa wangu’.” 26 Na pale pale walipoambiwa,“Ninyi si ‘watu wangu,’ ndipo watakapoitwa, ‘Wana wa Mungu aliye hai’.”