Salamu Kwa Watu Mbalimbali

16 Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika Kanisa la Kenkrea. Mpokeeni kama dada yenu katika Kristo, jinsi iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wow ote atakaohitaji kutoka kwenu maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, pamoja na mimi.

Salamu zangu kwa Priska na Akila, watumishi wenzangu katika huduma ya Kristo Yesu. Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Mimi ninawashukuru wao; na si mimi tu bali pia makanisa yote ya watu wa mataifa mengine. Natoa salamu pia kwa lile kanisa linaloabudu nyumbani kwao. Msalimuni rafiki yangu Epaineto aliyekuwa mtu wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.

Salamu zangu kwa Maria aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu. Wasalimuni Andronika na Yunia, jamaa zangu ambao wamekuwa gerezani pamoja nami. Wao ni maarufu miongoni mwa mitume, na walimfahamu Kristo kabla yangu. Salamu zangu kwa Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana. Salamu zangu kwa Urbano mfanyakazi mwenzetu katika utumishi wa Kristo pamoja na rafiki yangu mpendwa Stakisi. 10 Salamu zangu kwa Apele ambaye amethibitisha imani yake kwa Kristo. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani kwa Aristobulo. 11 Salamu zangu kwa ndugu yangu Herodioni, na kwa wote walio nyumbani kwa Narkisi wanaomwamini Bwana. 12 Salamu zangu kwa Trifainia na Trifosa, wakina mama wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana. Msalimuni mpendwa wangu Persisi ambaye pia ni mama mwingine aliyemtumikia Bwana kwa bidii. 13 Salamu zangu kwa Rufo, mteule wa Bwana na mama yake, ambaye amekuwa kama mama yangu pia. 14 Wasalimuni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao. 15 Salamu zangu kwa Filologona na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa na watu wote wa Mungu walio pamoja nao. 16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. Ndugu wa makanisa yote ya

Maonyo Ya Mwisho

17 Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na wote wanaoleta mafara kano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea. Waepukeni. 18 Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya, hupo tosha mioyo ya watu wanyofu. 19 Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na nimekuwa na furaha kwa ajili yenu. Lakini napenda muwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu. 20 Na Mungu wa amani hatakawia kumponda shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi. 21 Timotheo, mfanyakazi mwenzangu anawasalimu. Mnasalimiwa pia na Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu. 22 Na mimi Tertio niliyem wandishi wa barua hii nawasalimia kama ndugu yenu katika Kristo. 23 Salamu kutoka kwa Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote la hapa. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto pia wanawasalimu. [ 24 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amina].

Sala Ya Kumsifu Mungu

25 Na asifiwe Mungu ambaye anaweza kuwaimarisha katika Injili niliyowahubiria juu ya Yesu Kristo, kulingana na mafunuo ambayo yalikuwa yamefichika tangu zamani za kale; 26 lakini ambayo sasa yamewekwa wazi na kwa njia ya Maandiko ya manabii yamedhihirishwa kwa mataifa yote kwa amri ya Mungu wa milele, wapate kumwamini na kumtii. 27 Mungu aliye pekee mwenye hekima, atukuzwe milele na milele kwa njia ya Yesu Kristo! Amina.