Ninyi mnamtumikia Bwana Kristo. Mtu atendaye uovu atalipwa kwa uovu wake, wala hakuna atakayependelewa. Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu haki na ilivyo sawa mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni.

Maagizo Zaidi

Dumuni katika maombi, mkikesha na kushukuru. Pia tuom beeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango tupate kutoa ujumbe wetu na kuitangaza siri ya Kristo ambayo kwa ajili yake mimi nimefungwa gerezani. Ombeni kwamba niwezeshwe kuitangaza Injili kwa ufasaha, kama inipasavyo kusema.

Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkiutumia wakati wenu vizuri. Mazungumzo yenu yawe ya unyen yekevu wakati wote, yawe ya kuvutia, ili mjue jinsi ya kumjibu kila mtu.

Tikiko atawaelezeeni habari zangu zote. Yeye ni ndugu mpendwa, mfanyakazi mwaminifu na mtumishi mwenzangu katika Bwana. Nimemtuma kwenu kwa madhumuni kwamba mpate kufahamu hali yetu na pia awatie moyo. Anakuja pamoja na Onesmo ndugu yetu mpendwa na mwaminifu, ambaye ni mtu wa kwenu. Watawaelezeeni mambo yote yanayotendeka huku.

Salamu Na Maagizo Ya Mwisho

10 Aristarko aliyefungwa gerezani pamoja nami anawasalimu, hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, anawasalimu. Mmek wisha kupokea maagizo yanayomhusu. Akija kwenu, mpokeeni. 11 Na Yesu, yule aitwaye Yusto, pia anawasalimuni. Hawa tu, ndio Way ahudi kati ya watu tunaofanya nao kazi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu. 12 Epafra, ambaye ni mtu wa kwenu, na mtumishi wa Kristo Yesu , anawasalimu. Yeye anawaombea kwa bidii kila wakati kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu mkiwa mmekomaa na mkiwa thabiti. 13 Ninashuhudia kwamba anaomba kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na Hierapoli. 14 Luka, yule daktari mpendwa, pamoja na Dema, wanawasalimu. 15 Nisalimieni ndugu wote wa Laodikia na pia Nimfa pamoja na kanisa linalokutana nyumbani kwake.

16 Mkisha somewa barua hii, hakikisheni kuwa inasomwa pia na ndugu wa Laodikia. Na ninyi pia hakikisheni kuwa mnasoma barua inayotoka Laodikia.

17 Mwambieni Arkipo hivi: “Hakikisha kuwa unakamilisha ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana.”