23 Lakini hamna budi kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani yenu, pasipo kuyumba katika tumaini lililomo katika Injili. Hii ndio ile Injili mliyoisikia na ambayo imetan gazwa kwa kila kiumbe duniani na ambayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi wake.

Huduma Ya Paulo Kwa Makanisa

24 Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu na kwa mateso yangu ninakamilisha kile ambacho kimepungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa lake. 25 Mimi nime kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na wajibu niliopewa na Mungu, kuwasilisha kwenu neno la Mungu kwa ukamilifu.

Read full chapter