Wagalatia 3:24-6:17
Neno: Bibilia Takatifu
24 Kwa hiyo, sheria ilikuwa kama kiongozi wa kutufikisha kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 Lakini sasa kwa kuwa imani imekuja hatusimamiwi tena na sheria. 26 Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na
Wana Wa Mungu
4 Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. 2 Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 3 Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. 4 Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, 5 ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. 6 Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” 7 Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.
Paulo Alivyowajali Wagalatia
8 Zamani, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa mkitumikia ‘miu ngu’ ambayo kwa asili si miungu. 9 Lakini sasa kwa kuwa mmemfa hamu Mungu, au tuseme, sasa Mungu anawafahamu ninyi, mnawezaje kurudia tena upungufu na umaskini wa nguvu za pepo muwe watumwa wake? 10 Bado mnaadhimisha siku maalumu, miezi, nyakati na miaka! 11 Nina hofu juu yenu; inaelekea kazi niliyofanya kwa ajili yenu imepotea bure.
12 Ndugu zangu, nawasihi muwe kama mimi, kwa sababu na mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea ubaya wo wote. 13 Ninyi mnafahamu kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia nafasi ya kuwa hubiria Habari Njema kwa mara ya kwanza. 14 Lakini ninyi hamku nidharau wala kunikataa ingawa udhaifu wa mwili wangu ulikuwa mzigo kwenu. Bali mlinipokea vizuri kama malaika wa Mungu, na kama Kristo Yesu. 15 Ile furaha mliyokuwa nayo iko wapi sasa? Naweza kushuhudia kwamba wakati ule mlikuwa tayari hata kung’oa macho yenu mnipe. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu nawaambieni ukweli?
17 Hao watu wanaoshughulika ili muwe upande wao nia yao si nzuri. Wanataka kuwatenganisha na sisi ili muwajali wao zaidi. 18 Ni vema watu wanapowahangaikia kwa bidii kama shabaha ya kufanya hivyo ni nzuri, na kama wanafanya hivyo wakati wote, isiwe tu wakati nikiwa nanyi. 19 Watoto wangu wadogo, najisikia kwa mara nyingine kama mama mwenye uchungu wa kuzaa, nikitamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20 Natamani ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha msemo wangu. Kwa maana nata tanishwa na hali yenu.
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kutawaliwa na sheria, je, hamu elewi sheria inavyosema? 22 Kwa maana imeandikwa katika Maandi ko kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mtoto mmoja alizal iwa na mwanamke mtumwa, na wa pili alizaliwa na mwanamke huru. 23 Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili na yule wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu. 24 Mambo haya yanaweza kueleweka kama mfano. Kwa maana hao mama wawili ni mfano wa maagano mawili: agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika mlima wa Sinai, wakazaliwa watoto wa utumwa; huyo ni Hajiri. 25 Hajiri sasa anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabuni, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26 Lakini Yerusalemu ya mbinguni ni huru, nayo ndio mama yetu. 27 Kwa maana imeandikwa: “Furahi wewe uliyetasa usiyeweza kuzaa; piga kelele, ulie kwa furaha wewe usiyepatwa na maumivu ya uzazi; kwa maana watoto wa yule ali yeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.”
28 Sasa ndugu zangu, sisi kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivy omtesa yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 30 Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mwanamke mtumwa pamoja na mwanae; kwa sababu mtoto wa mtumwa hawezi kurithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.” 31 Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mwanamke huru. Uhuru Ndani Ya Kristo
5 Kristo alituweka sisi huru ili tuwe na uhuru. Kwa hiyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na minyororo ya utumwa. 2 Sikilizeni! Mimi Paulo nawaambieni kwamba kama mkiku bali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia cho chote. 3 Tena, napenda kumshuhudia kila mmoja wenu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria zote. 4 Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria fahamuni kwamba mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5 Kwa maana, kwa msaada wa Roho wa Mungu, sisi tunangojea kwa matumaini kupata haki kwa njia ya imani. 6 Kwa maana tukiwa ndani ya Kristo, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuleti faida yo yote, bali jambo la msingi ni kuwa na imani inayofanya kazi kwa upendo.
7 Mlikuwa mkienenda vizuri, sasa ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8 Kushawishiwa huku hakutokani na yule anayewaita. 9 Hamira kidogo sana inaweza kuchachusha donge zima. 10 Nina hakika katika Bwana kwamba mtakubaliana na msimamo wangu. Huyo anayewasumbueni atapata hukumu anayostahili hata akiwa nani. 11 Lakini ndugu zangu, kama mimi ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini bado nateswa? Ingekuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingekuwa kikwazo tena. 12 Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!
13 Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili muwe watu huru. Hata hivyo msitumie uhuru wenu kuendelea kufuata tamaa za mwili, bali tumi kianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 14 Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 15 Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana, basi jihadhar ini, msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe.
Maisha Ya Kiroho
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18 Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria.
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.
24 Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake. 25 Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26 Tusiwe watu wenye maji vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo
6 Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. 2 Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. 3 Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. 4 Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5 Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. 6 Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.
7 Msidanganyike, Mungu hadanganywi. Kwa maana kila mtu ata vuna kile alichopanda. 8 Mtu apandaye katika tamaa za mwili, ata vuna kutoka katika mwili uharibifu; lakini yeye apandaye katika Roho, atavuna kutoka katika Roho uzima wa milele. 9 Basi, tusi choke kutenda mema, kwa sababu kama hatukuchoka tutavuna kwa wakati wake. 10 Kwa hiyo basi, kadiri tunavyopata nafasi, tuwa tendee mema watu wote, na hasa wale tunaoshiriki imani moja.
Maonyo Ya Mwisho Na Salamu
11 Tazameni jinsi maandishi ya mkono wangu mwenyewe yalivyo makubwa. 12 Ni wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaowalazimisheni mtahiriwe; na wanafanya hivyo ili wao wenyewe wasije kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo. 13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawashiki sheria; lakini wanataka na ninyi mtahiriwe ili wapate kujivunia hiyo alama katika miili yenu. 14 Lakini mimi kamwe sitajivunia kitu cho chote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; kwa maana kwa njia ya msalaba, ulimwengu umesulubiwa kwangu, na mimi nimesulubiwa kwa ulimwengu. 15 Kwa maana, kutahiriwa au kutota hiriwa si kitu kwangu; kitu cha maana ni maisha ya watu kubadili ika kuwa mapya. 16 Amani na rehema ya Mungu ikae na wote wanao fuata kanuni hii, na kwa Israeli ya kweli ya Mungu.
17 Basi, tangu sasa mtu ye yote asije akanisumbua, kwa sababu ninazo alama za Yesu mwilini mwangu.
Wagalatia 3:24-4:11
Neno: Bibilia Takatifu
24 Kwa hiyo, sheria ilikuwa kama kiongozi wa kutufikisha kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 Lakini sasa kwa kuwa imani imekuja hatusimamiwi tena na sheria. 26 Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na
Wana Wa Mungu
4 Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. 2 Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 3 Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. 4 Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, 5 ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. 6 Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” 7 Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.
Paulo Alivyowajali Wagalatia
8 Zamani, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa mkitumikia ‘miu ngu’ ambayo kwa asili si miungu. 9 Lakini sasa kwa kuwa mmemfa hamu Mungu, au tuseme, sasa Mungu anawafahamu ninyi, mnawezaje kurudia tena upungufu na umaskini wa nguvu za pepo muwe watumwa wake? 10 Bado mnaadhimisha siku maalumu, miezi, nyakati na miaka! 11 Nina hofu juu yenu; inaelekea kazi niliyofanya kwa ajili yenu imepotea bure.
Matendo Ya Mitume 15:1-21
Neno: Bibilia Takatifu
Wayahudi. 28 Wakakaa huko na wale wanafunzi kwa muda mrefu.
Baraza La Yerusalemu
15 Watu wengine walikuja Antiokia kutoka Yudea wakawa wakiwa fundisha ndugu walioamini kwamba, “Kama hamkutahiriwa kufuatana na desturi iliyofundishwa na Musa hamwezi kuokolewa.” 2 Paulo na Barnaba walikuwa na mabishano makali nao wakipinga mafundisho haya. Ikaamuliwa kwamba Paulo na Barnaba na waamini wengine waende Yerusalemu wakawaulize mitume na wazee juu ya jambo hili. 3 Kwa hiyo, wakiwa wametumwa na kanisa, njiani walipitia makanisa ya Foenike na Samaria wakatoa taarifa jinsi watu wa mataifa men gine walivyokuwa wakimgeukia Bwana. Habari hizi ziliwafurahisha sana hao ndugu. 4 Walipofika Yerusalemu walipokelewa na kanisa, mitume na wazee; nao wakatoa taarifa kuhusu mambo yote ambayo Mungu aliyafanya kwa kuwatumia wao. 5 Lakini baadhi ya waamini waliokuwa wakishikilia desturi za Mafarisayo wakasema, “Ni lazima watahiriwe na wafundishwe kushika sheria ya Musa.”
6 Mitume na wazee wa kanisa wakakutana kushauriana juu ya jambo hili. 7 Baada ya majadiliano marefu, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za mwanzo Mungu alini chagua ili kwa midomo yangu watu wa mataifa mengine wapate kusi kia Habari Njema na kuamini. 8 Na Mungu ambaye anajua mioyo ya watu alishuhudia kwamba anawakubali watu wa mataifa kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa na sisi. 9 Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa sababu waliamini. 10 Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hawa ndugu wanafunzi mzigo wa sheria ambao baba zetu na sisi tumesh indwa kuubeba? 11 Sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Yesu, kama na wao wanavyookolewa.” 12 Baraza lote likakaa kimya; wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa mataifa. 13 Walipomaliza maelezo yao, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. 14 Simoni amekwisha kutueleza jinsi, kwa mara ya kwanza, Mungu amejichagulia waamini kutoka kwa watu wa mataifa. 15 Hata maneno ya manabii yanakubaliana kabisa na jambo hili. Kama ilivyoandikwa: 16 ‘ Baada ya mambo haya nitarudi, nami nitajenga upya nyumba ya Daudi ambayo imeanguka. Nitajenga tena magofu yake na kuisimamisha, 17 ili binadamu wengine wote wamtafute Bwana, pamoja na watu wa mataifa yote ambao wanaitwa kwa jina langu; 18 asema Bwana, ambaye ametufahamisha mambo hayo tangu kale.’
19 “Kwa hiyo uamuzi wangu ni kwamba, tusiwasumbue watu wa mataifa wanaomgeukia Mungu kwa desturi zetu; 20 badala yake, tuwaandikie barua tuwaambie wajiepushe na uchafu wa ibada za sanamu, na zinaa na waache kula nyama ya wanyama walionyongwa au kunywa damu. 21 Kwa maana sheria za Musa zimekuwa zikihubiriwa katika kila mji na kusomwa katika masinagogi kila sabato tangu vizazi vya awali.”
Read full chapter

Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica