Wagalatia 3:1-11
Neno: Bibilia Takatifu
Kuhesabiwa Haki Kwa Njia Ya Imani
3 Ninyi Wagalatia wajinga! Nani aliyewaloga? Yesu Kristo alielezwa wazi wazi mbele yenu kwamba alisulubiwa. 2 Nataka mni jibu swali moja: je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kutimiza sheria au kwa kuamini mliyosikia? 3 Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Baada ya kuanza na Roho wa Mungu, sasa mnataka kuwa wakamilifu kwa uwezo wenu wenyewe? 4 Je, mateso yote yaliyowapata hayakuwa faa kitu? Kweli yalikuwa bure? 5 Je, Mungu anawapa Roho wake na kufanya miujiza kati yenu kwa sababu mnatii sheria au kwa sababu mnaamini Injili mliyosikia?
6 Tazameni mfano wa Abrahamu: “Yeye alimwamini Mungu, na Mungu alimhesabu kuwa mtu mwenye haki.” 7 Kwa hiyo mnaona kwamba watu wanaomwamini Mungu ndio watoto halisi wa Abrahamu. 8 Na Maandiko yalitabiri mambo ya baadaye, kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa mengine kwa njia ya imani. Kwa hiyo Maandiko yalitangulia kumtangazia Abrahamu kwa kutamka, “Kwa ajili yako mataifa yote yatabarikiwa.” 9 Hivyo basi, walio na imani wana barikiwa pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa mtu wa imani.
Sheria Na Laana
10 Wote wanaotegemea kutimiza sheria, wako chini ya laana. Kwa sababu Maandiko yanasema, “Mtu ye yote asiyeshika na kufu ata mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, amelaani wa.” 11 Ni wazi kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kutimiza sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.”
Read full chapter

Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica