Wana Wa Mungu

Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.

Paulo Alivyowajali Wagalatia

Zamani, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa mkitumikia ‘miu ngu’ ambayo kwa asili si miungu. Lakini sasa kwa kuwa mmemfa hamu Mungu, au tuseme, sasa Mungu anawafahamu ninyi, mnawezaje kurudia tena upungufu na umaskini wa nguvu za pepo muwe watumwa wake? 10 Bado mnaadhimisha siku maalumu, miezi, nyakati na miaka! 11 Nina hofu juu yenu; inaelekea kazi niliyofanya kwa ajili yenu imepotea bure.

12 Ndugu zangu, nawasihi muwe kama mimi, kwa sababu na mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea ubaya wo wote. 13 Ninyi mnafahamu kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia nafasi ya kuwa hubiria Habari Njema kwa mara ya kwanza. 14 Lakini ninyi hamku nidharau wala kunikataa ingawa udhaifu wa mwili wangu ulikuwa mzigo kwenu. Bali mlinipokea vizuri kama malaika wa Mungu, na kama Kristo Yesu. 15 Ile furaha mliyokuwa nayo iko wapi sasa? Naweza kushuhudia kwamba wakati ule mlikuwa tayari hata kung’oa macho yenu mnipe. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu nawaambieni ukweli?

17 Hao watu wanaoshughulika ili muwe upande wao nia yao si nzuri. Wanataka kuwatenganisha na sisi ili muwajali wao zaidi. 18 Ni vema watu wanapowahangaikia kwa bidii kama shabaha ya kufanya hivyo ni nzuri, na kama wanafanya hivyo wakati wote, isiwe tu wakati nikiwa nanyi. 19 Watoto wangu wadogo, najisikia kwa mara nyingine kama mama mwenye uchungu wa kuzaa, nikitamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20 Natamani ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha msemo wangu. Kwa maana nata tanishwa na hali yenu.

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kutawaliwa na sheria, je, hamu elewi sheria inavyosema? 22 Kwa maana imeandikwa katika Maandi ko kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mtoto mmoja alizal iwa na mwanamke mtumwa, na wa pili alizaliwa na mwanamke huru. 23 Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili na yule wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu. 24 Mambo haya yanaweza kueleweka kama mfano. Kwa maana hao mama wawili ni mfano wa maagano mawili: agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika mlima wa Sinai, wakazaliwa watoto wa utumwa; huyo ni Hajiri. 25 Hajiri sasa anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabuni, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26 Lakini Yerusalemu ya mbinguni ni huru, nayo ndio mama yetu. 27 Kwa maana imeandikwa: “Furahi wewe uliyetasa usiyeweza kuzaa; piga kelele, ulie kwa furaha wewe usiyepatwa na maumivu ya uzazi; kwa maana watoto wa yule ali yeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.”

28 Sasa ndugu zangu, sisi kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivy omtesa yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 30 Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mwanamke mtumwa pamoja na mwanae; kwa sababu mtoto wa mtumwa hawezi kurithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.” 31 Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mwanamke huru. Uhuru Ndani Ya Kristo

Ninalolisema ni hili: Wakati mrithi wa vyote alivyomiliki baba yake bado ni mdogo, hana tofauti yo yote na mtumwa. Haijalishi kuwa anamiliki vitu vyote. Wakati wa utoto bado anapaswa kuwatii wale waliochaguliwa kumtunza. Lakini anapoufikia umri ambao baba yake ameuweka, anakuwa huru. Ndivyo ilivyo hata kwetu sisi. Mwanzoni tulikuwa kama watoto, tukiwa watumwa wa mamlaka za uovu[a] zinazoutawala ulimwengu huu wa sasa. Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu akamtuma Mwanaye, aliyezaliwa na mwanamke na akaishi chini ya sheria. Mungu alifanya hivi ili aweze kuwaweka huru wale waliokuwa chini ya sheria. Kusudi la Mungu lilikuwa kutuasili[b] sisi kama watoto wake.

Ninyi sasa ni watoto wa Mungu. Na ndiyo sababu Mungu amemtuma Roho wa Mwanaye mioyoni mwetu. Huyo Roho aliye ndani yetu hulia “Aba,[c] yaani Baba.” Sasa ninyi si watumwa kama mwanzo. Ni watoto wa Mungu, na mtapokea kila kitu ambacho Mungu aliwaahidi watoto wake. Hii yote ni kwa sababu ya yale ambayo Mungu amewatendea ninyi.

Upendo wa Paulo kwa Waamini wa Galatia

Zamani hamkumjua Mungu. Mlikuwa watumwa wa miungu isiyokuwa halisi. Lakini sasa mnamjua Mungu wa kweli. Hakika, Mungu ndiye anayewajua ninyi. Hivyo kwa nini sasa mnavigeukia vikosi dhaifu na visivyo na manufuaa yoyote mlivyovifuata hapo mwanzo? Mnataka kuwa watumwa wa mambo haya tena? 10-11 Inanipa wasiwasi kwa kuwa mnaadhimisha siku, miezi, misimu na miaka. Nina hofu ya kuwa nimefanya kwa bidii kazi bure kwa ajili yenu.

12 Ndugu zangu, naomba mniige mimi kama ambavyo mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunikosea kwa jambo lololote. 13 Mnajua kuwa nilikuja kwenu mara ya kwanza kwa sababu nilikuwa mgonjwa. Ndipo nilipowaeleza ninyi Habari Njema. 14 Ugonjwa wangu uliwaelemea. Hata hivyo hamkunikataa kutokana na fadhaa ama hofu. Bali, mlinikaribisha kama vile nilikuwa malaika kutoka kwa Bwana. Mlinipokea kama vile nilikuwa Kristo Yesu mwenyewe! 15 Mlikuwa na furaha sana wakati huo. Nini kimetokea kwa imani yenu ya awali kwamba mimi nilikuwa mtu niliyebarikiwa kipekee na Mungu? Naweza kusema bila shaka yoyote kwamba mngeliweza kufanya kitu chochote kunisaidia. Kama ingeliwezekana, mngeliyang'oa hata macho yenu na kunipa mimi. 16 Je, nimekuwa sasa adui yenu kwa sababu nawaambia ukweli?

17 Watu hawa[d] wanajitahidi sana kuonesha kuvutiwa nanyi,[e] lakini hiyo siyo nzuri kwenu. Wanataka kuwashawishi ninyi ili mtugeuke sisi na kuambatana nao. 18 Inapendeza daima kuwa na mtu anayevutiwa nawe katika jambo lililo jema. Hivyo ndivyo nilivyofanya nilipokuwa pamoja nanyi. Siku zote inapendeza, na si pale tu mimi nikiwapo. 19 Watoto wangu wadogo, nasikia uchungu tena kwa ajili yenu, kama mama anayejifungua. Nitaendelea kusikia uchungu huu mpaka watu watakapofikia kumwona Kristo wawatazamapo ninyi. 20 Natamani ningekuwa nanyi sasa. Ndipo labda ninapoweza kubadilisha namna ninavyoongea nanyi. Sasa sielewi nifanye nini juu yenu.

Mfano wa Hajiri na Sara

21 Baadhi yenu mnataka kuwa chini ya sheria. Niambieni, mnajua sheria inavyosema? 22 Maandiko yanasema kwamba Ibrahimu alikuwa na wana wawili. Mama wa mwana mmoja alikuwa ni mjakazi, na mama wa mwana mwingine alikuwa wa mwanamke aliye huru. 23 Mwana wa Ibrahimu kutoka kwa mjakazi alizaliwa kwa namna ya kawaida ya kibinadamu. Lakini mwana kutoka kwa mwanamke aliyekuwa huru alizaliwa kwa sababu ya ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu.

24 Habari hii ina maana nyingine kwenu. Wanawake wawili ni sawa na maagano mawili baina ya Mungu na watu wake. Agano moja ni sheria ambayo Mungu aliifanya katika Mlima Sinai, inayowafanya watu wawe watumwa. Mwanamke aliyeitwa Hajiri yuko kama agano la kwanza. 25 Hivyo Hajiri anauwakilisha Mlima Sinai uliopo Arabia. Na anafanana na Yerusalemu wa sasa, kwa sababu mji huu uko utumwani pamoja na watu wake. 26 Lakini Yerusalemu ya mbinguni ulio juu uko kama mwanamke aliye huru, ambaye ndiye mama yetu. 27 Maandiko yanasema,

“Ufurahi mwanamke, wewe uliye tasa.
    Ufurahi kwani hukuwahi kuzaa.
Piga kelele na ulie kwa furaha!
    Hukupata uchungu wa kuzaa.
Mwanamke aliye peke yake atapata watoto zaidi
    zaidi ya mwanamke aliye na mume.”(A)

28 Ndugu zangu, ninyi ni watoto mliozaliwa kwa sababu ya ahadi ya Mungu, kama Isaka alivyozaliwa. 29 Lakini mwana mwingine wa Ibrahimu, aliyezaliwa kwa njia ya kawaida, alisababisha matatizo kwa yule aliyezaliwa kwa nguvu ya Roho. Ndivyo ilivyo leo. 30 Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mjakazi na mwanawe! Mwana wa mwanamke aliye huru atapokea kila kitu alicho nacho baba yake, lakini mwana wa mjakazi hatapokea kitu.”(B) 31 Hivyo, kaka na dada zangu, sisi si watoto wa mjakazi. Ni watoto wa mwanamke aliye huru.

Footnotes

  1. 4:3 mamlaka za uovu Ina maana pia ya nguvu za giza.
  2. 4:5 kutuasili Ina maana ya kutufanya watoto wake na kutupa haki zote.
  3. 4:6 Aba Ni neno la Kiaramu lililotumiwa na watoto wa Kiyahudi kama jina la kuwaita baba zao.
  4. 4:17 Watu hawa Walimu wa uongo waliokuwa wanawasumbua waamini kule Galatia. Tazama Gal 1:7.
  5. 4:17 kuvutiwa nanyi Ina maana ya “wanakereketwa sana kwa mambo yenu”.