13 Naweza kufanya mambo yote katika yeye anipaye nguvu.

14 Hata hivyo, mlifanya vizuri kunisaidia kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. 15 Ninyi ndugu zangu Wafilipi mnajua kwamba nilipoanza kuhubiri Injili, nilipokuwa natoka Makedonia, hakuna kanisa lililoshirikiana nami katika kutoa na kupokea isi pokuwa ninyi.

Read full chapter