16 Hawa wanahubiri kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba Mungu ameniweka hapa kifungoni ili niitetee Injili. 17 Hao wengine wanamtangaza Kristo kwa tamaa ya kupata sifa wala si kwa moyo wa upendo, wakifikiri kwamba kwa kufanya hivyo wataniongezea mateso yangu kifungoni. 18 Lakini kwangu mimi hiyo si kitu. Lililo la muhimu ni kwamba kwa kila njia Kristo anahubiriwa, ikiwa kwa nia mbaya au kwa nia njema. Kwa sababu hiyo, mimi nashangilia. Pia nitaendelea kushan gilia,

Read full chapter