Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana kufanya hivyo ni vizuri. “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” Akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana. Watumwa Na Mabwana

Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. Nanyi mabwana watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme simama. 14 Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; 15 na kuvaa Injili ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara. 16 Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. 17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. 18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu. 19 Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. 20 Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo. 21 Ndugu mpendwa Tikiko, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawaelezeni kila kitu ili mjue habari zangu na mfahamu ninachofanya. 22 Ninamtuma kwenu kwa kusudi hili, mpate habari zetu naye awafariji. 23 Nawatakia ndugu wote amani na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.