Waefeso 5:22-33
Neno: Bibilia Takatifu
22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi
Read full chapter

Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica