Waefeso 4:4-16
Neno: Bibilia Takatifu
4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, k ama mlivyoitwa mpokee tumaini moja. 5 Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; 6 na Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wot e, aliye juu ya wote, anayefanya kazi katika yote na aliye ndani ya yote. 7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo alichogawiwa na Kristo. 8 Kwa hiyo Maandiko yanasema: “Alipopaa juu, aliongoza mateka wengi, na akawapa watu zawadi.” 9 Maandiko yanaposema, “Alipaa juu’ 10 Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sana, kupita mbingu zote, ili apate kujaza vitu vyote. 11 Yeye ndiye aliyewapa watu vipawa, wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu; 12 wapate kuwatayarisha watu wa Mungu kwa kazi za huduma, kwa ajili ya kujenga kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo. 13 Kazi hiyo itaende lea mpaka sote tuufikie umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu; tupate kuwa watu waliokomaa kiroho kwa kufikia kiwango cha ukamilifu wote ulio ndani ya Kristo. 14 Hapo ndipo tutaacha kuwa tena kama watoto wadogo, wanaorushwarushwa huku na huko na kupeperushwa na kila upepo wa mafundisho na hila za watu wadan ganyifu. 15 Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica