16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. 17 Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, 18 mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo; 19 na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe. 20 Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu. 21 Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina.

Read full chapter