Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo. Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe; na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake. Kutoka kwake, tunapata ukombozi kwa ajili ya damu yake, yaani, kusamehewa dhambi zetu; kulingana na wingi wa neema yake ambayo ametumiminia kwa wingi. Kwa maana ametufahamisha kwa hekima yote na ufahamu, siri ya mapenzi yake, kulingana na mpango aliokusudia kuukamilisha kwa njia ya Kristo. 10 Mpango huo ambao ungetekelezwa wakati ukitimia, ni kwamba Mungu ataviunganisha vitu vyote po pote vilipo, mbinguni na duniani, viwe kwake chini ya Kristo. 11 Tukiwa ndani ya Kristo, tulichaguliwa kama alivy opanga Mungu kwa makusudio yake yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake. 12 Kwa njia hiyo, sisi ambao tulikuwa wa kwanza kumtegemea Kristo, tupate kuishi maisha yatakayoleta sifa kwa utukufu wake. 13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho Mtakatifu ambaye mliahidiwa, 14 yeye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoupokea, kwa sifa ya utukufu wake. Shukrani Na Maombi

Read full chapter