Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa akionyesha kwamba maadamu hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa bado haijafunguliwa. Hii ili kuwa ni kielelezo kwa wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizotolewa zilikuwa haziwezi kutakasa dhamiri ya mtu anayeabudu. 10 Hizi zilikuwa ni sheria zinazohusu chakula na vinywaji na taratibu mbalimbali za utakaso wa nje, kanuni ambazo zingetumika mpaka wakati wa matayarisho ya utaratibu mpya.

Read full chapter