Add parallel Print Page Options

Lakini Mungu aligundua kitu kilichokuwa na kasoro kwa watu, akasema:

“Wakati unakuja, asema Bwana,
    nitakapofanya agano jipya na watu wa Israeli na watu wa Yuda.
Halitakuwa sawa na agano lililotengenezwa na baba zao.
    Hilo ni agano nililowapa nilipowachukua kwa mkono na kuwatoa Misri.
Hawakuendelea kufuata agano nililowekeana nao,
    na nikageuka mbali nao, asema Bwana.
10 Hili ni agano jipya nitakalofanya
    na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana:
Nitaziweka sheria zangu katika fahamu zao,
    na nitaandika sheria zangu katika mioyo yao.
Nitakuwa Mungu wao,
    nao watakuwa watu wangu.

Read full chapter