Lakini Mungu hakurid hika na watu wake, akasema, “Siku zinakuja, asema Bwana, nitaka pofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao siku ile nilipowashika mkono niwaongoze kutoka nchi ya Misri; kwa kuwa hawakuwa waaminifu kwa agano langu, nami nikawaacha, asema Bwana. 10 Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli siku zile zitakapowadia, asema Bwana: nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

Read full chapter