11 Tunapenda kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyo hiyo mpaka mwisho ili mpate kupo kea tumaini lenu. 12 Hatutaki muwe wavivu bali muige wale ambao kwa imani na subira hupokea yale yaliyoahidiwa na Mungu.

Uhakika Wa Ahadi Ya Mungu

13 Mungu alipompa Ibrahimu ahadi, aliapa kwa jina lake mwe nyewe kwa kuwa hapakuwa na mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake.

Read full chapter