Tuige Mfano Wa Yesu

12 Basi na sisi kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi inay otusonga kwa urahisi; tupige mbio kwa ustahimilivu katika mashin dano yaliyowekwa mbele yetu. Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu. Yeye, kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, alivumilia kifo cha msalaba bila kujali aibu, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

Mtafakarini yeye aliyestahimili uadui wa namna hii kutoka kwa wenye dhambi; msije mkachoka wala kufa moyo. Katika kushin dana kwenu na dhambi, bado hamjapigana na majaribu kiasi cha kufikia hatua ya kumwaga damu yenu. Je, mmekwisha sahau yale maneno ya kuwatia moyo, yanayowataja kama wana? “Mwanangu, usid harau nidhamu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya. Maana Bwana huwaadhibu wale awapendao na humpiga kila anayemkubali kuwa ni mwanae.”

Vumilieni mateso kama mafunzo. Mungu anawatendea kama wanawe. Maana ni mwana yupi asiyeadhibiwa na baba yake? Kama mtaachiwa bila kuwa na nidhamu, na kila mtu hufundishwa kuwa na nidhamu, basi ninyi ni wana haramu, si wanawe wa halali. Zaidi ya hayo, baba zetu waliotuzaa walituadhibu nasi tukawaheshimu kwa ajili hiyo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa baba wa roho zetu ili tuishi? 10 Baba zetu wa hapa duniani walituadhibu kwa muda mfupi kama wao wenyewe walivyoona kwamba inafaa. Lakini Mungu anatuadhibu kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11 Adhabu yo yote huonekana kuwa kitu cha kuumiza na kisichofu rahisha wakati ule inapotolewa. Lakini baadaye, matunda yake kwa wale waliofundishwa kwa nidhamu hiyo, ni haki na amani.

12 Kwa hiyo imarisheni mikono yenu iliyolegea na magoti yenu yaliyo dhaifu. 13 Nyosheni njia za miguu yenu ili mguu ulioumia usilemae, bali upone.

14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na utaka tifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana. 15 Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu, na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua ikaleta matatizo na kuwachafua wengi. 16 Hakik isheni kwamba miongoni mwenu hamna mwasherati au mtu asiyemcha Mungu. Kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja, aliuza haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza. 17 Maana mnafahamu ya kwamba baadaye, alipotaka kurithi ile baraka aliyokuwa apewe, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.

18 Hamkuja kukaribia mlima ambao unaweza kuguswa, na ambao unawaka moto; wala hamkuja kwenye giza, huzuni na dhoruba, 19 na mlio wa tarumbeta na sauti ikisema maneno kwa kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno lingine zaidi. 20 Kwa maana hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Kama hata mnyama atag usa mlima huu, atapigwa mawe.” 21 Kwa hakika waliyoona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” 22 Lakini ninyi mmekuja kwenye Mlima wa Sioni, na kwenye mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni, ambapo wamekusanyika kwa shangwe maelfu na maelfu ya malaika. 23 Mmefika kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu ambao majina yao yameandikwa mbin guni. Mmekuja mbele ya Mungu, hakimu wa watu wote, na mbele ya roho za watu wenye haki, waliofanywa wakamilifu. 24 Mmefika kwa Yesu, msuluhishi wa agano jipya, na kwa damu ile iliyonyunyizwa, inenayo maneno mema kuliko damu ya Abeli.

25 Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa hawa kuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi tutaepukaje tukimkataa yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 26 Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”

27 Maneno haya, “Kwa mara moja tena,” yanaonyesha kwamba vile vinavyotetemeshwa vitaondolewa, yaani vyote vilivyoumbwa, kusudi vibaki vile tu visivyoweza kutetemeshwa.

28 Kwa hiyo, tuwe na shukrani kwa kuwa tumepokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna itakay ompendeza, kwa unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto unaoteketeza.

Mwenendo Wa Mkristo

13 Endeleeni kupendana kama ndugu. Msiache kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivyo watu wengine waliwakaribisha mal aika pasipo kujua. Wakumbukeni waliofungwa gerezani kama vile mmefungwa pamoja nao; pia wakumbukeni wanaoteswa, kwa kuwa na ninyi bado mnaishi katika mwili.

Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.

Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha.” Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu, sitaogopa kitu, mwanadamu anaweza kunifanya nini?”

Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Tafakarini jinsi walivyoishi na matokeo ya mwenendo wao, mkaige imani yao. Yesu Kristo ni yule yule, jana, leo na hata milele. Msipotoshwe na mafundisho ya kigeni ya namna mbalimbali. Ni vema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, na wala si kwa kutii mash arti kuhusu vyakula, ambavyo havina faida kwa wanaovila. 10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema ya kuabudia hawana haki ya kula vitu vilivyowekwa juu yake.

11 Nyama za hao wanyama ambao damu yao huletwa na kuhani mkuu katika Patakatifu pa Patakatifu kama dhabihu ya dhambi, huchomwa nje ya kambi. 12 Kwa hiyo Yesu naye aliteswa nje ya mlango wa mji ili awatakase watu kwa damu yake. 13 Kwa hiyo tum wendee nje ya kambi, tukashiriki aibu aliyostahimili. 14 Maana hapa hatuna mji wa kudumu, bali tunautafuta ule mji ujao.

15 Basi, kwa njia ya Yesu, tuendelee kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo ya watu wanaokiri jina lake. 16 Msiache kutenda mema na kushirikiana mlivyo navyo, kwa maana sadaka kama hizi ndizo zinazompendeza Mungu.

17 Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

18 Tuombeeni, kwa maana tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi na tunapenda kufanya yaliyo sawa daima. 19 Ninawasihi zaidi mniombee ili nirudishwe kwenu upesi zaidi.

Sala

20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, 21 awape ninyi kila kitu chema, ili mpate kutimiza mapenzi yake akifanya ndani yenu lile linalopendeza machoni pake, kwa njia ya Yesu Kristo; yeye apewe utukufu milele na milele.

Maneno Ya Mwisho

22 Basi, ndugu zangu, nawasihi mpokee vema maonyo haya, maana nimewaandikia kwa ufupi.

23 Napenda kuwafahamisha kwamba ndugu yetu Timotheo amefun guliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja naye kuwaona.

24 Wasalimuni viongozi wenu wote pamoja na watu wote wa Mungu. Salamu zenu kutoka kwa ndugu wa Italia.