Imani

11 Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni uhakika wa mambo tusiyoyaona. Maana ni kwa imani wazee wa kale walipata kibali cha Mungu.

Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vinavyoonekana vilitengenezwa kutokana na vitu visiv yoonekana.

Kwa imani Abeli alimtolea Mungu sadaka bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alikubaliwa kuwa mtu mwenye haki, Mungu aliposi fia sadaka zake. Na kwa imani yake bado anasema ingawa amekufa.

Kwa imani, Enoki alichukuliwa mbinguni ili asife, hakuone kana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Basi, kabla haja chukuliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu. Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa bidii.

Kwa imani Noe alipoonywa na Mungu kuhusu mambo yaliyokuwa hayajaonekana bado, alitii akajenga safina kuokoa jamii yake. Kwa sababu hii aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatika nayo kwa imani.

Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende kwenye nchi ambayo Mungu angempa kama urithi. Naye aliondoka akaenda ingawa hakujua aendako. Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi ya ahadi. Aliishi katika nchi ya ugenini katika mahema pamoja na Isaki na Yakobo ambao pia walikuwa warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akitazamia mji wenye misingi ya kudumu ambao umebuniwa na kujengwa na Mungu mwenyewe.

11 Kwa imani Sara alipewa uwezo wa kupata mimba ijapokuwa alishapita umri wa kuzaa, kwa sababu aliamini kwamba Mungu ali yemwahidi ni mwaminifu na angelitimiza ahadi yake. 12 Kwa hiyo kutokana na huyu mtu mmoja, ambaye alikuwa sawa na mfu, walizal iwa wazao wengi kama nyota za mbinguni na kama mchanga usiohesa bika wa pwani.

13 Watu wote hawa walikuwa bado wanaishi kwa imani walipo kufa. Hawakupata yale waliyoahidiwa; lakini waliyaona na kuyafu rahia kwa mbali. Nao walikiri kwamba walikuwa ni wageni wasiokuwa na maskani hapa duniani. 14 Maana watu wanaosema maneno kama hayo, wanaonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Kama walikuwa wakifikiria kuhusu nchi waliyoiacha, wangali pata nafasi ya kurudi huko. 16 Lakini sasa wanatamani nchi iliyo bora zaidi, yaani, nchi ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa maana amewatayarishia mji.

17 Kwa imani Abrahamu alipojaribiwa alimtoa Isaki awe dha bihu. Yeye ambaye alikuwa amepokea ahadi za Mungu alikuwa tayari kumtoa mwanae wa pekee awe dhabihu, 18 ingawa Mungu alikuwa amemwambia, “Uzao wako utatokana na Isaki.” 19 Abrahamu aliamini kwamba Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu, na kweli ni kama alimpata tena Isaka kutoka katika kifo.

20 Kwa imani Isaki aliwabariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yatakayotokea baadaye.

21 Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea kichwa cha ile fimbo yake.

22 Kwa imani Yosefu alipokuwa amekaribia mwisho wa maisha yake, alitaja habari za kutoka kwa wana wa Israeli huko Misri, na akatoa maagizo kuhusu mifupa yake.

23 Kwa imani Mose alipozaliwa alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mwenye umbo zuri, wala hawakuogopa amri ya mfalme.

24 Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao, 25 badala yake akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu, kuliko kufurahia anasa za dhambi za kitambo kidogo. 26 Aliona kwamba kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni uta jiri mkubwa zaidi kuliko hazina ya Misri; maana alikuwa anataza mia kupata tuzo baadaye. 27 Kwa imani Mose alitoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme, kwa maana alivumilia kama amwonaye yeye asiyeonekana. 28 Kwa imani aliitimiza Pasaka na kunyunyiza damu ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.

29 Kwa imani watu wakavuka Bahari ya Shamu kama vile juu ya nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo, wakafa maji.

30 Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka, watu walipozizunguka kwa siku saba.

31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi.

32 Basi niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kuwaeleza habari za Gidioni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii. 33 Hawa, kwa imani walishinda milki za wafalme, walite keleza haki, walipokea ahadi za Mungu, walifunga vinywa vya simba; 34 walizima moto mkali, na waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini wakatiwa nguvu, walikuwa hodari vitani, wakafukuza majeshi ya kigeni yakakimbia. 35 Wanawake walipokea wapendwa wao waliokuwa wamekufa wakafufuliwa. Lakini wengine wal iteswa wakakataa kufunguliwa, ili wapate kufufukia maisha bora zaidi. 36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata wakafungwa pingu na kutiwa gerezani. 37 Walipigwa mawe, walikatwa vipande viwili kwa misumeno, waliuawa kwa panga, walizurura wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, walikuwa maskini, waliteswa na kutendewa mabaya. 38 Ulimwengu haukustahili kuwa na watu kama hao: walizungukazunguka jangwani, katika milima na katika mapango na mashimo ardhini.

39 Na wote hawa, ingawa walishuhudiwa vema kwa sababu ya imani yao, hawakupokea yale waliyoahidiwa, 40 kwa sababu Mungu alikuwa amepanga kitu bora zaidi kwa ajili yetu, kwamba wasinge likamilishwa pasipo sisi.