Ukuu Wa Mwana Wa Mungu

Hapo zamani Mungu alisema na baba zetu mara nyingi na kwa namna mbali mbali kwa kuwatumia manabii. Lakini katika siku hizi za mwisho, amesema na sisi kwa njia ya Mwanae, ambaye alim chagua kuwa mrithi wa vitu vyote. Na kwa njia ya Mwanae, Mungu aliumba ulimwengu. Yeye Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa halisi ya nafsi yake, naye huudumisha na kuuendeleza ulim wengu kwa neno lake lenye nguvu. Alipokwisha kuwapatia wanadamu utakaso wa dhambi, alikaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi aliye juu. Kwa hiyo Mwana alikuwa mkuu zaidi kuliko malaika, kama ambavyo jina alilorithi kwa Mungu ni kuu kuliko jina la malaika ye yote.

Kwa maana ni malaika gani ambaye Mungu aliwahi kumwambia: “Wewe ni mwanangu; leo hii nimekuzaa”? Au tena: “Mimi nita kuwa Baba yake na yeye atakuwa Mwanangu”? Na tena Mungu ana pomleta mwanae, mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anasema: “Malaika wote wa Mungu wamwabudu yeye.” Anapozungumza juu ya malaika anasema: “Anawafanya malaika wake kuwa upepo, watumishi wake kuwa ndimi za moto.” Lakini kuhusu Mwana, anasema: “Kiti chako cha enzi, Wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na haki takuwa fimbo ya ufalme wako. Umependa haki na kuchukia uovu. Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuchagua wewe na kukuweka juu ya wenzako kwa kukupaka mafuta ya furaha.” 10 Pia anasema: “Hapo mwanzo , Wewe Bwana, uliweka misingi ya ulimwengu, na mbingu ni kazi ya mikono yako. 11 Vyote vitaangamia lakini wewe unadumu; vyote vitachakaa kama nguo, nawe 12 utavikunja kama vazi na kuvibadilisha. Bali wewe hubadiliki, na miaka yako haitakwisha kamwe. ” 13 Lakini ni malaika gani amewahi kumwambia, “Keti kulia kwangu mpaka niwafanye adui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako”? 14 Malaika ni nani basi? Wao ni roho wa utumishi waliotumwa kuwahudumia wale watakaopokea wokovu.