Font Size
Ufunuo 3:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 3:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
10 Umeifuata amri yangu kwa uvumilivu. Hivyo nitakulinda wakati wa shida itakayokuja ulimwenguni, wakati ambapo kila aishiye duniani atajaribiwa.
11 Naja upesi. Ishikilie imani uliyonayo, ili mtu yeyote asiichukue taji yako. 12 Wale watakaoshinda watakuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu. Hawataliacha hekalu la Mungu tena. Nitaandika juu yao jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu. Mji huo ni Yerusalemu mpya.[a] Unateremka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika jina langu jipya juu yao.
Read full chapterFootnotes
- 3:12 Yerusalemu mpya Mji wa kiroho ambako Mungu ataishi pamoja na watu wake.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International