Add parallel Print Page Options

Mnyama kutoka Baharini

13 Kisha niliona mnyama mwenye pembe kumi na vichwa saba akipanda kutoka baharini. Kila pembe yake ilikuwa na taji. Alikuwa na kumkufuru Mungu lililoandikwa kwenye kila kichwa. Mnyama huyu alionekana kama chui, miguu yake ilikuwa kama ya dubu. Mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Joka akampa huyo mnyama uweza wake wote, kiti chake cha enzi na mamlaka kuu.

Kichwa kimoja cha mnyama kilionekana kama kimejeruhiwa na kuuawa, lakini kidonda cha mauti kilipona. Watu wote ulimwenguni walishangaa, na wote walimfuata mnyama.

Read full chapter