Font Size
Ufunuo 1:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 1:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
5 na kutoka kwa Yesu Kristo aliye shahidi mwaminifu. Aliye wa kwanza miongoni mwa watakaofufuliwa kutoka kwa wafu na ndiye mtawala wa wafalme wote wa dunia.
Yesu ndiye anayetupenda na ametuweka huru na dhambi zetu kwa sadaka ya damu yake. 6 Ametufanya sisi kuwa ufalme wake na makuhani wanaomtumikia Mungu, Baba yake. Utukufu na nguvu viwe kwa Yesu milele na milele! Amina.
7 Tazama, Yesu anakuja pamoja na mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma.[a] Watu wote wa dunia watamwombolezea.[b] Ndiyo, hili litatokea! Amina.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Copyright © 2017 by Bible League International