Add parallel Print Page Options

Nani anaweza kukifungua kitabu?

Kisha niliona kitabu[a] katika mkono wa kulia wa aliyekaa kwenye kiti cha enzi. Kitabu hiki kilikuwa na maandishi pande zote na kilikuwa kimefungwa kwa mihuri saba. Na nikamwona malaika mwenye nguvu, aliyeita kwa sauti kubwa, “Ni nani anayestahili kuivunja mihuri na kukifungua kitabu?” Lakini hakukuwa yeyote mbinguni au duniani au chini ya dunia ambaye angeweza kukifungua kitabu na kutazama ndani yake. Nililia sana kwa sababu hakuwepo aliyestahili kukifungua kitabu na kuangalia ndani yake. Lakini mmoja wa wazee akaniambia, “Usilie! Simba[b] kutoka kabila la Yuda ameshinda. Ni mzaliwa wa Daudi. Anaweza kukifungua kitabu na mihuri yake saba.”

Kisha nikamwona Mwanakondoo amesimama katikati karibu na kiti cha enzi kilichozungukwa na viumbe wanne wenye uhai. Wazee pia walikuwa wamemzunguka Mwanakondoo aliyeonekana kama aliyeuawa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambayo ni roho saba za Mungu zilizotumwa ulimwenguni kote. Mwanakondoo alikuja na akakichukua kile kitabu kutoka katika mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwenye kiti enzi. Baada ya Mwanakondoo kukichukua kile kitabu, viumbe wenye uhai wanne na wazee ishirini na wanne wakainama mbele za Mwanakondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi. Pia walikuwa wameshikilia bakuli za dhahabu zilizojaa ubani, ambao ni maombi ya watu watakatifu wa Mungu. Na wote walimwimbia wimbo mpya Mwanakondoo:

“Unastahili kukichukua kitabu
    na kuifungua mihuri yake,
kwa sababu uliuawa,
    na kwa sadaka ya damu yako uliwanunua watu kwa ajili ya Mungu,
    kutoka kila kabila, lugha, rangi na taifa.
10 Uliwafanya kuwa ufalme na makuhani kwa ajili ya Mungu wetu.
    Nao watatawala duniani.”

11 Kisha, nilipotazama, nikasikia sauti ya malaika wengi waliozunguka kiti cha enzi pamoja na viumbe wenye uhai wanne na wazee ishirini na nne. Walikuwa maelfu kwa maelfu ya malaika, elfu kumi mara elfu kumi. 12 Kwa sauti kuu malaika walisema:

“Mamlaka yote, utajiri, hekima na nguvu ni kwa Mwanakondoo aliyeuawa.
    Anastahili kupokea heshima, utukufu na sifa!”

13 Ndipo nikasikia kila kiumbe kilichoumbwa kilichoko mbinguni na duniani na chini ya dunia na baharini, viumbe vyote sehemu hizo vikisema:

“Sifa zote na heshima
    na utukufu na nguvu kuu ni kwa ajili yake Yeye aketiye
    kwenye kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo milele na milele!”

14 Viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wazee wakainama chini wakasujudu.

Footnotes

  1. 5:1 Hapa inamaanisha hati ndefu ya kukunja kwa kuvingirisha (ni vitabu vilivyotumika zamani). Katika Biblia unapoona neno kitabu au vitabu, inamaanisha hati hizi.
  2. 5:5 Simba Imetumika hapa kumaanisha Yesu.

Hati Na Mwana-Kondoo

Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwe nye kile kiti cha enzi hati iliyoandikwa ndani na nje, ambayo ilikuwa imefungwa na mihuri saba. Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, “Ni nani anayestahili kufungua hati hii na kuvunja mihuri yake?” Lakini hakupatikana mtu mbinguni, juu ya nchi, wala chini ya nchi aliyeweza kufungua hati hiyo, wala kuitazama. Nililia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kuifungua hati hiyo wala kuitazama. Kisha, mmoja wapo wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, yule simba wa kabila la Yuda, wa ukoo wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kufun gua hati hiyo na kuvunja mihuri yake saba.” Katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wanne na wale wazee, nikaona Mwana- Kondoo amesimama, akionekana kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba, na macho saba, ambayo ni wale roho saba wa Mungu waliotumwa ulimwenguni kote . Huyo Mwana-Kondoo akaenda, akaichukua ile hati kutoka kwenye mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. Alipokwisha kuichukua ile hati, wale viumbe wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ubani , ambao ni maombi ya watu wa Mungu. Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.” 11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti za mal aika wengi sana wakizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi ya hao mal aika ilikuwa ni maelfu na maelfu na kumi elfu mara kumi elfu. 12 Nao waliimba kwa sauti kuu, “Mwana -Kondoo aliyeuawa anasta hili kupewa uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima, na utukufu na sifa!” 13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, juu ya nchi na chini ya nchi, baharini na vyote vilivy omo baharini wakiimba, “Baraka na heshima na utukufu na uweza ni wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi; na kwa Mwana-Kondoo, hata milele na milele! 14 Na wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi wakaabudu.