Ndipo nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa bwana wake. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Tazama, maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, naye atakuwa Mungu wao. Atafuta machozi yao yote, na kifo hakitakuwepo tena, wala maom bolezo, wala kilio, wala maumivu; maana mambo hayo yote ya awali yamekwisha toweka.”

Read full chapter