Ujumbe Kwa Kanisa La Efeso

“Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: ‘Haya ni maneno ya yule aliyeshika nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu. Najua matendo yako, bidii yako na uvumilivu wako. Najua kuwa huwezi kuvumilia watu waovu na kwamba umewapima wale wanaojiita mitume na kumbe sio, na umetambua ya kuwa wao ni waongo. Najua umevumilia na kustahimili mateso kwa ajili ya jina langu, wala hujachoka .

Lakini nina neno hili juu yako: kwamba umeacha upendo wako wa kwanza. Kumbuka pale ulipokuwa kabla ya kuanguka. Tubu, uache dhambi zako, ukafanye matendo ya mwanzo. Kama hukuacha dhambi zako, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. Lakini una jambo moja zuri: unayachukia matendo ya Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.

Mwenye nia ya kusikia na ayasikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa . Atakayeshinda, nitampa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ambao uko katika bustani ya Mungu.”’

Ujumbe Kwa Kanisa La Smirna

“Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye wa kwanza na wa mwisho; aliyekufa kisha akawa hai tena.

Naijua dhiki yako na umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri! Najua matukano wanayokutukana wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi; wao ni sinagogi la shetani. 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuhakikishia kuwa shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu. Nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

11 Mwenye nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa. Atakayeshinda hatadhuriwa na kifo cha pili.’ ”

Ujumbe Kwa Kanisa La Pergamo

12 “Kwa malaika wa Kanisa la Pergamo andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili.

13 Ninajua unakoishi, kule ambako shetani ameweka kiti chake cha enzi. Hata hivyo umelishika jina langu, wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambao ni maskani ya shetani.

14 Lakini nina mambo machache juu yako: baadhi yenu ni wafu asi wa mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki awashaw ishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na kufanya uasherati. 15 Na tena baadhi yenu wanafu ata mafundisho ya Wanikolai. 16 Basi tubuni mwache dhambi zenu: ama sivyo nitakuja hivi karibuni na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.

17 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho ana waambia makanisa. Atakayeshinda nitampa sehemu ya ile mana iliy ofichwa, nami nitampa jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.’

Ujumbe Kwa Kanisa La Thiatira

18 “Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika hivi: ‘Haya ni maneno ya Mwana wa Mungu ambaye macho yake ni kama moto uwakao, na miguu yake inang’aa kama shaba iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua matendo yako, upendo wako, imani yako, huduma na subira yako; na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya mwanzo.

20 Hata hivyo ninalo jambo hili juu yako: unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kwa miungu. 21 Nimempa muda atubu, aache uasher ati, lakini hataki kutubu. 22 Kwa hiyo nitamtupa kitandani kwa ugonjwa, na atapata mateso makali pamoja na hao wanaozini naye wasipotubu matendo yake. 23 Tena nitawaua watoto wake. Ndipo makanisa yote yatajua kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na akili za watu na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Lakini ninawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamfuati mafundisho ya Yezebeli, wala ham kujifunza hayo wengine wanayoyaita ‘siri za ndani’ za shetani, sitawaongezea mzigo mwingine. 25 Bali mshike sana hicho mlicho nacho mpaka nitakapokuja.

26 Atakayeshinda na kuendelea kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa. 27 ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunja vipande vipande kama chombo cha udongo 28 Pia nitampa ile nyota ya asubuhi. 29 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaambia makanisa.’ ”