Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai walianguka kifudifudi wakamwabudu Mungu aliyekuwa ameketi katika kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu, “Amina! Hale luya!”

Na sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Msi funi Mungu wetu ninyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”

Kisha nikasikia sauti kama sauti ya umati mkubwa wa watu, kama sauti ya maporomoko ya maji mengi na kama ngurumo kuu ya radi kubwa ikisema, “Haleluya! Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwe nyezi anatawala.

Read full chapter