Kuanguka Kwa Babiloni

18 Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni akiwa na uwezo mkuu. Ulimwengu wote uliangazwa kwa utu kufu wake. Naye akasema kwa sauti kuu, “Ameanguka, Babiloni mkuu, ameanguka! Amekuwa maskani ya mashetani, makazi ya kila roho mchafu, kiota cha kila ndege mchafu na wa kuchukiza. Maana mataifa yote yamekunywa divai ya uasherati wake, na wafalme wa duniani wamezini naye; na wafanya biashara wa duniani wametaji rika kutokana na tamaa yake mbaya isiyo na mipaka.”

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, tokeni kwake msije mkashiriki dhambi zake mkapati kana na maafa yatakayompata; maana dhambi zake zimelundikana hadi mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. Mtendee kama yeye alivyotenda, umlipe mara mbili zaidi kwa matendo yake; mchanganyie kinywaji mara mbili zaidi ya kile kinywaji alicho changanya. Kama yeye alivyojitukuza kwa uasherati wake, mpe mateso na maombolezo kwa kipimo hicho hicho. Kwa kuwa kama ase mavyo moyoni mwake, ‘Mimi naketi kama malkia, si mjane wala sita pata msiba kamwe.’ Hivyo ndivyo maafa yatakavyomjia kwa siku moja; tauni na msiba na njaa, naye atachomwa kwa moto; kwa maana amhukumuye ni Bwana Mungu mwenye uweza.

Na wafalme wa mataifa waliozini naye na kushiriki tamaa zake watalia na kuomboleza watakapoona moshi wa kuungua kwake. 10 Watasimama mbali kwa hofu ya mateso yake na kusema, “Ole wako! Ole wako, mji mkuu, Babiloni, mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!” 11 Na wafanya biashara wa duniani watalia na kuomboleza kwa maana hakuna anunuaye bidhaa zao tena. 12 Bidhaa za dhahabu, fedha, vito vya thamani na lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarao, hariri, na nguo nyekundu, aina zote za mti wa udi, vifaa vya meno ya tembo, vifaa vyote vya mbao ya thamani, shaba, chuma na marumaru, 13 mdalasini, hiliki, uvumba, marhamu, ubani, divai, mafuta ya mzeituni, unga mzuri, ngano, ng’ombe, kondoo, farasi na magari, na watumwa, pia na roho za wanadamu. 14 Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliy atamani yametoweka, na utajiri wako wote na ufahari vimetoweka, wala hutavipata kamwe!’

15 Wale wafanya biashara wa bidhaa hizo waliopata utajiri wao kwake watasimama mbali kabisa kwa kuogopa mateso yake, nao watalia na kuomboleza kwa nguvu wakisema, 16 ‘Ole wako! Ole wako! mji mkuu, ulikuwa umevikwa mavazi ya kitani safi, rangi ya zambarau na nyekundu, uking’aa kwa dhahabu na vito vya thamani na lulu! 17 Katika muda wa saa moja utajiri wote huu umeharibiwa!’ Manahodha wote, mabaharia na wote wasafirio baharini na wote wafanyao kazi melini watasimama mbali kabisa.

18 Watakapoona moshi wake wakati mji ukiteketezwa watalia wakisema, ‘Kuna mji gani ambao umepata kuwa kama mji huu mkuu?’ 19 Nao watajimwagia vumbi vichwani na kulia na kuomboleza wakisema, ‘Ole wako, Ole wako mji mkuu, mji ambapo wote wenye meli baharini walitajirika kwa mali yake! Maana katika saa moja tu umeteketezwa. 20 Fura hini juu yake, enyi mbingu, watakatifu na mitume na manabii; Kwa kuwa Mungu ameuhukumu kwa ajili yenu!”’

21 Kisha malaika mkuu akachukua jiwe kama jiwe kubwa la kusagia akalitupa baharini akisema, ‘ ‘Hivyo ndivyo mji mkuu wa Babiloni utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana kamwe. 22 Wala sauti za wapiga vinanda, na wapiga zomari, wapiga fil imbi na sauti ya wapiga tarumbeta hazitasikika kwako kamwe. Hata patikana kwako fundi mwenye ujuzi wo wote; wala sauti ya jiwe la kusaga haitasikika kamwe. 23 Na nuru ya taa haitaangaza ndani yako tena; Wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako kamwe. Maana wafanya biashara wako walikuwa watu maarufu wa duniani, na mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako. 24 Na ndani yake ilikutwa damu ya manabii na watakatifu na watu wote waliouawa duniani.”