Na kwenye kipaji cha uso wake yaliandikwa maneno yenye maana iliyofichika: “Babiloni Mkuu, Mama wa Makahaba na wa Machukizo yote ya Duniani.” Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa damu ya watu wa Mungu na damu ya watu waliouawa kwa kumshuhudia Yesu. Nilipomwona, nilistaajabu sana. Lakini yule malaika akaniambia, “Kwa nini unastaajabu? Nitakufunulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyembeba, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

Read full chapter