Mnyama Kutoka Baharini

13 Kisha nikaona mnyama akitoka baharini. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba na taji kumi kwenye pembe zake. Na kila kichwa kiliandikwa jina la kufuru. Huyo mnyama alifanana kama chui lakini miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka lilimpa mnyama huyo nguvu zake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu. Kichwa kimoja cha huyo mnyama kilione kana kama kilikwisha kuwa na jeraha lisiloweza kupona, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona na dunia nzima ilimstaajabia huyo mnyama na kumfuata. Watu waliliabudu lile joka kwa sababu lili kuwa limempa huyo mnyama uwezo wake. Pia walimwabudu huyo mnyama wakisema, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”

Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujisifu na ya kufuru na akapewa haki ya kutawala kwa muda wa miezi arobaini na miwili. Alisema maneno ya kumkufuru Mungu, akilitukana jina lake na mahali aishipo, yaani, aliwatukana wale waishio mbinguni. Pia aliruhusiwa kuwapiga vita watu wa Mungu na kuwashinda. Alipewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, kila ukoo, kila lugha na taifa. Na watu wote waishio duniani watamwabudu, yaani kila mmoja ambaye tangu kabla ya ulimwengu kuumbwa, jina lake haliku andikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa.

“Aliye na nia ya kusikia, asikilize kwa makini: 10 Ye yote aliyepangiwa kuchukuliwa mateka atatekwa. Mtu ye yote akiua kwa upanga atauawa kwa upanga. Na hii ndio nafasi ya watu wa

Mnyama Kutoka Ardhini

11 Kisha nikamwona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika ardhi. Alikuwa na pembe mbili kama za mwana kondoo lakini aliongea kama joka. 12 Naye alitumia uwezo wote wa yule mnyama wa kwanza aliyemtangulia. Akalazimisha dunia yote na wote waliomo duniani wamwabudu huyo mnyama wa kwanza aliyekuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona. 13 Huyu mnyama wa pili akafanya miu jiza ya ajabu hata kufanya moto utoke mbinguni na kushuka duniani mbele ya watu. 14 Kwa njia ya miujiza aliyowezeshwa kufanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, aliwadanganya watu waishio duniani. Aliwaamuru watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 15 Kisha akawe zeshwa kuipatia pumzi ile sanamu ya mnyama wa kwanza hata ikaweza kuongea na kufanya wale wote ambao hawakuiabudu wauawe. 16 Pia aliwalazimisha watu wote, wakubwa kwa wadogo, matajiri na mas kini, watu huru na watumwa, watiwe alama kwenye mikono yao ya kulia au kwenye vipaji vya nyuso zao. 17 Hakuna mtu ye yote ambaye angeweza kununua au kuuza kitu kama hana alama ile, yaani jina la huyo mnyama au namba ya jina lake.

18 Jambo hili linahitaji hekima. Mwenye akili ya kutambua apige hesabu ya mnyama huyo kwa sababu ni namba ya mtu. Namba yake ni mia sita sitini na sita.