Mnyama Kutoka Baharini

13 Kisha nikaona mnyama akitoka baharini. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba na taji kumi kwenye pembe zake. Na kila kichwa kiliandikwa jina la kufuru. Huyo mnyama alifanana kama chui lakini miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka lilimpa mnyama huyo nguvu zake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu. Kichwa kimoja cha huyo mnyama kilione kana kama kilikwisha kuwa na jeraha lisiloweza kupona, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona na dunia nzima ilimstaajabia huyo mnyama na kumfuata.

Read full chapter