Mwanamke Na Joka

12 Ndipo ishara kuu ikaonekana mbinguni: palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa juu ya kichwa chake. Alikuwa mjam zito,akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kujifungua. Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. Mkia wake ulifagia theluthi moja ya nyota zote angani na kuziangusha ardhini. Joka hili likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kujifungua, likiwa tayari kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. Mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto huyo akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu, kwenye kiti chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambako Mungu alik wisha kumtengenezea mahali pa kumtunza kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.

Vita Mbinguni

Kisha kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake waki pigana na hilo joka. Joka nalo pamoja na malaika wake likapigana nao. Lakini joka na malaika wake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni. Basi joka hilo kuu likatupwa nje, yule nyoka wa kale aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye watu wote ulimwenguni. Alitupwa chini ardhini, yeye pamoja na malaika wake.

Ushindi Mbinguni Watangazwa

10 Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, “Sasa umeti mia wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake yamefika. Kwa kuwa mshtaki wa ndugu zetu anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana ametupwa chini. 11 Nao wamemshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao, kwa kuwa wao hawakuyapenda maisha yao kiasi cha kuogopa kifo. 12 Kwa hiyo furahini ninyi mbingu, na wote wakaao mbinguni! Bali ole wenu nchi na bahari maana shetani amekuja kwenu akiwa amejaa ghadhabu, kwa maana anajua kuwa muda wake ni mfupi!”

13 Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilim winda yule mwanamke aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume. 14 Lakini huyo mama akapewa mabawa mawili ya yule tai mkubwa kusudi aruke hadi mahali ambapo atatunzwa kwa muda na nyakati na nusu ya wakati. 15 Lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, mafuriko yakamfuata huyo mama ili yamchukue. 16 Lakini ardhi ikamsaidia huyo mama; ikafunua kinywa chake na kuumeza ule mto uliotoka kinywani mwa joka. 17 Kisha lile joka likashikwa na ghadhabu kwa ajili ya huyo mama, likaondoka kwenda kupigana vita na watoto wake waliobakia, wale wanaozitii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.