Malaika Mwenye Hati Ndogo

10 Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa amevaa wingu, na upinde wa mvua kich wani. Uso wake uling’aa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto. Mkononi mwake alikuwa ameshika hati ndogo iliyokuwa imefunguliwa. Mguu wake wa kulia aliuweka juu ya bahari na mguu wake wa kushoto aliuweka juu ya nchi kavu. Naye akaita kwa sauti kuu kama simba anayenguruma. Alipopaza sauti, ngurumo saba ziliitikia kwa kishindo. Na zile ngurumo saba zilipokwisha kuitikia, nilitaka kuanza kuandika, lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Funga hayo yaliyosemwa na ngurumo hizo saba, ni siri; usiyaandike.”

Kisha yule malaika aliyekuwa amesimama juu ya bahari na nchi kavu akainua mkono wake wa kulia juu mbinguni, akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo, na bahari na vyote vilivy omo, akasema, “Wakati wa kungoja umekwisha. Lakini katika siku ambazo yule malaika wa saba atakaribia kupiga tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa kama alivyowatangazia watumishi wake manabii.”

Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia pale mwanzoni ikasema nami tena, “Nenda, kachukue ile hati iliyoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na nchi kavu.”

Basi nikaenda, nikamwomba yule malaika anipe ile hati ndogo. Akaniambia, “Ichukue uile. Itakuwa chungu tumboni mwako, lakini mdomoni mwako itakuwa tamu kama asali.” 10 Basi nikaichukua ile hati ndogo kutoka mkononi mwa yule malaika nikaila. Ilikuwa tamu kama asali mdomoni mwangu lakini nili poimeza, ikawa chungu tumboni mwangu. 11 Kisha nikaambiwa, “Inakubidi kutoa unabii tena kuhusu watu wengi, na mataifa, lugha na wafalme.”